Breaking News

Your Ad Spot

Jul 29, 2010

CORPORATE GOLF DAY 2010

Hii ni kuwahabarisha kuwa, siku ya jumamosi ya tarehe 31 kutakuwa na Press conference itakayofanyika viwanja vya Gymkhana club,posta.

Press conference hii inahusu Corporate Golf Day, itakayofanyika tarehe 14 ya mwezi wa nane, palepale Gymkhana,ikiwahusisha wafanyakazi wa makampuni mbalimbali watakaoshindana katika mchezo wa golf.

Vilevile, Kutakuwa na zoezi la mnada wa vitu mbalimbali kama vyumba vya kulala pale Movenpick, Harbour View na Kempinski,...modem za internet, tiketi za ndege, na Live cooking BBQ itakayoandaliwa na Hillside Hotel, Bagamoyo. Mapato ya mnada huu yatapatiwa kwa Gymkhana Golf Club kwa ajili ya kuandaa mazoezi na mafunzo ya golf kwa watoto na vijana wanaocheza Golf.

Watakaoongea katika press conference hii ni Oscar Shelukindo-TBL, Emillian Rwejuna- Precision Air, Mr. Nyirabu- Mwenyekiti wa Dar Gymkhana Club, na Mariam Ndabagenga- Muandaaji wa shughuli hii kupitia Brand Image Ltd.

Wote mnakaribishwa,

Ahsante

Mariam Iddi Ndabagenger
Marketing Manager
Brand Image Ltd
+255 713 299 678
+255 787 028 658
mariam.ndaba@gmail.com

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages