Breaking News

Your Ad Spot

Aug 14, 2010

JK AONGOZA KIKAO CHA CHA HALMASHAURI KUU YA CHAMA MJINI DODOMA, AAGA MABALOZI WAPYA WA TANZANIA NCHINI UFARANSA NA MAREKANI


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongoza kikao cha halmashauri kuu ya CCm Taifa mjini Dodoma leo asubuhi.Wengine katika picha kutoka kushoto ni Rais Mstaafu awamu ya Tatu Benjamin William Mkapa, Rais Mstaafu awamu ya pili Mzee Ali Hassan Mwinyi,Makamu wa CCM Bara Pius Msekwa na kulia nia katibu mkuu wa CCM Yusuf Makamba.(picha na Freddy Maro).
 Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Waziri Mkuu Mizengo Pinda muda mfupi kabla ya kuanza kwa kikao cha Halmshauri Kuu ya  CCM Taifa mjini  Dodoma leo asubuhi.Katikati ni Katibu mkuu wa CCM  Yusuf Makamba.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Balozi mpya wa Tanzania nchini Ufaransa Mhe. Begum Taj wakati balozi huyo na mwenzake Balozi Mwanaidi Maajar(kulia) walipokwenda kumuaga ikulu ndogo mjini Dodoma leo asubuhi.Balozi Mwanaidi Maajar aliyekuwa balozi wa Tanzania nchini Uingereza anakuwa balozi wa Tanzania nchini Marekani na kituo chake cha kazi kitakuwa Washington.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages