Breaking News

Your Ad Spot

Aug 13, 2010

VODA YATOA VIFAA VYA MICHEZO KWA KLABU ZA DARAJA LA KWANZA

KLAB 12 zitakazoshiriki katika msimu huu wa ligi kuu TANZANIA BARA vimekabidhiwa vifaa vya michezo vyenye thamani ya shilingi MILIONI MIA MBILI TISINI kutoka kwa mdhamini mkuu wa ligi hiyo kampuni ya simu za mkononi VODACOM.
Wakati wa makabidhiano hayo yalishuhudiwa na viongozi wa vilabu na wa TFF ambao ni makamu wa pili wa rais wa (TFF) RAMADHAN NASIBU na kaimu katibu mkuu ambaye pia ni mkurugenzi wa ufundi SUNDAY KAYUNI wa shirikisho hilo.
Ni wiki moja imebaki kuanza kwa msimu wa ligi kuu sokaTanzania bara ambapo hatua ya awali ya kukabidhi vifaa kwa vilabu hivyo imefanyika ikihusisha viatu ,jezi na mipira kwaajili ya matayarisho na vifaa vitakavyotumika wakati wa mashindano hayo.
Wakati wa hafla hiyo, Mkuu wa udhamini wa kampuni hiyo GEORGE RWEHUMBIZA amesema kampuni yake imetenga kiasi cha shilingi BILIONI MOJA kudhamini ligi hiyo kati ya hizo shilingi MILIONI MIA SITA SABINI zimetengwa kwa ajili ya shughuli za uendeshaji
Naye mkurugenzi wa masoko wa kampuni hiyo, EPHRAIM MAFURU amesema kampuni yake imeamua kuongeza udhamini wa ligi hiyo ili kusaidia wachezaji waweze kufanya vizuri katika michezo yao na hivyo kuwa ni ligi ya ushindani.
Baada ya makabidhiano hayo makamu wa pili wa rais wa TFF, RAMADHANI NASIBU alivitaka vilabu kuonyesha upinzani katika msimu huu wa ligi ili kuvutia zaidi wadhmani ,huku baadhi ya viongozi waliofika kuchukua vifaa hivyo wakiipongeza kampuni ya VODACOM kwa kutoa vifaa vyenye ubora
Ligi kuu Tanzania bara inatarajia kuanza kutimua vumbi AUGOST 21 katika viwanja tofauti hapa nchini lakini itatanguliwa na mchezo wa NGAO ya HISANI kati ya bingwa mtetezi wa ligi hiyo SIMBA dhidi ya YANGA uliopangwa kufanyika AUGOST 18.
EPHRAIM Mafuru kulia mkurugenzi wa masoko vodacom pamoja na GOERGE RWEHUMBIZA mkuu wa udhamini vodacom na NECTOR FOYA meneje mawasiliano VODACOM wakati wa kukabidhi vifaa vya michezo kwa vilabu vinavyoshiriki ligi kuu TANZANIA BARA
 Vi

Vifaa vikikabidhiwa timu ya Yanga
Vifaa vikikabidhiwa timu ya Simba
  
Vifaa vikikabidhiwa timu ya Ruvu shooting

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages