Breaking News

Your Ad Spot

Aug 12, 2010

TIMU YA TAIFA YA POOL YAPATA KOCHA MZAMBIA

CHAMA cha mchezo wa Pool Table Tanzania (TAPA) kwa kushirikiana na mdahamini mkuu wa mchezo huo hapa nchini, bia ya Safari Lager inayotengenezwa na kampuni ya Bia Tanzania (TBL) leo imemtambulisha rasmi Denis Lungu kutoka Zambia kuwa kocha mkuu wa timu ya taifa ya mchezo huo.


Akimtambulisha kwa waandishi wa habari katika kijiji cha Makumbvusho ya Taifa, Kijitonyama, Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa TAPA Amios Kafwinga, kafwinga alisema, atafundisha timu ya taifa ya pool hapa nchini kwa mkata wa miaka miwili kuanzia Agosti 1, 2010 hadi Julai 28, 2012.


Kafwinga alisema kuletwa kwa kocha huyo ni kwa mujibu wa katiba ya chama hicho inayoelekeza kwamba kitasimamia na  kuendelea mchezo wa pool. "kwa kuzingatia jukumu hilo zito chama cha Pool Tanzania, kwa kushirikiana na mdhamini mkuu wa mchezo huo, Bia ya  Safari Lager tumeamua kumleta kocha huyu. Hatua hii itawezesha kuhakikisha mchezo wa pool hapa nchini unachezwa katika kiwango cha juu", alisema.


Naye Mwenyekiti wa TAPA,  Isack Togocho amewaasa wachezaji wa timu ya taifa na wale watakaoteuliwa katika timu hiyo wamtumie vyem,a kocha huyo kukuza viwango vyao vya uchezaji ili hatimaye waweze kusajiliwa katika vilabu vya kulipwa nje ya nchi.


Alimshukuru meneja wa Bia ya Safari Lager  Fimbo Butala kwa kuwa bega kwa bega na kutoa ushirikiano mkubwa katika kuhakikisha mchezo wa pool unakuwa na hadhi inayostahili hapa nchioni.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages