Breaking News

Your Ad Spot

Sep 16, 2010

CORPORATE GOLF DAY 2010

Press Release

CORPORATE GOLF DAY, 24th SEPTEMBER 2010.

Dar es Salaam Wednesday, September 15, 2010 –

 Brand Image Limited pamoja na wadhamini wake, wametangaza leo kuwepo kwa Corporate Golf Day, inayotegemewa kufanyika tarehe 24th September 2010,katika viwanja vya golf vya Gymkhana.

Ikiwa kama kampuni inayojihusisha na masuala ya kukuza Mahusiano ya makampuni mbalimbali kwa kupitia michezona shughuli nyingine mbalimbali, Brand Image inayapatia makampuni binafsi nafasi ya kujenga mahusiano mazuri baina yao, kukuza brand zao pamoja na kupimana nguvu katika mchezo wa golf.

Wazungumzaji katika habari maelezo iliyofanyika jumatano tarehe 15, walikuwa wawakilishi kutoka Pepsi, Ecobank, Harbour View, MGen Insurance, Brand Image, na Gymkhana golf club. Hata hivyo, shughuli hii imeandaliwa na Brand Image na kudhaminiwa na DT Dobie, Stanbic Bank, TBL, PEPSI SBC, Harbour View, MGen Insurance, Zantel, Aggrey & Clifford, CHOICE FM, Vodacom, The Citizen, Standard Chartered Plc, Precision Air, Tanzania Distillers Limited, Ecobank na Clouds FM;

Wawakilishi kutoka Gymkhana Golf Club waliwashukuru sana Brand Image Ltd kwa kuwaunga mkono katika kazi zao, na wakatoa changamoto kwa makampuni mengine kuungana na kampuni hii ya Brand Image katika kukuza na kuendeleza michezo Tanzania.

Mchezo huu wa Corporate Golf utafanyika katika viwanja vya Gymkhana, siku ya Ijumaa tarehe 24th September 2010, kuanzia saa tatu asubuhi mpaka saa nne usiku.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages