MGOMBEA Urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM),Dk. Jakaya Kikwete, akisalimiana na wananchi wa Haydom, mkoani Manyara, alipowasili katika mkutano wa kampeni, jana.(Picha na Freddy Maro).
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi, Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Mwenyekiti wa Chipukizi wa Mkoa wa Manyara Hilda Prosper Hinghmaghway (7), anayesoma darasa la pili katika shule ya Rift Valley iliyoko Babati wakati wa mkutano wa kampeni wa CCM uliohutubiwa na Mgombea urais kupitia chama hicho mjini Babati, jana. (Picha na John Lukuwi).
MGOMBEA urais kwa tiketi ya CCM, Rais Jakaya Kikwete akiagana na wananchi kwa kuwapungua mkono, baada ya kuhutubia mkutano wa kampeni jana, wilayani Babati. icha na John Lu(P kuwi).
MWENYEKITI wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo Tanzania (WAMA), Mama Salma Kikwete, akiwanadi wagombea Ubunge kwa tiktei ya CCM, Dk. Charles Tizeba (Buchosa) na William Ngeleja ( Sengerema), akiwa katika ziara yake ya kampeni za CCM mkoani Mwaanza, juzi. (Picha na Mwanakombo Jumaa-Maelezo).
Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi UVCCM) Taifa, Ridhiwani Kikwete akisalimiana na wafuasi wa chama hicho, alipofika Kata ya Msimbati, Mtwara vijijini kufungua tawi la UVCCM jana.(Picha na Richard Mwaikenda)
Ridhiwani Kikwete akiwa na mwalimu aliyemsomesha darasa la kwanza 1987 katika Shule yaMsingi Matangini Sophia Makong'o, alipomtembelea nyumbani kwake mjini Nachingwea juzi,Kulia ni mtoto wa Makong'o, Husna ambaye alisoma naye Ridhiwani darasa la kwanza katika shule hiyo. (Picha na Richard Mwaikenda)
Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi UVCCM) Taifa, Ridhiwani Kikwete akipandisha bendera ya chama hicho wakati wa uzinduzi wa Tawi jipya la Namindondi wakati wa ziara ya kampeni ya kupanga mikakati ya ushindi wa chama hicho katika mkutanio Mkuu, juzi katika Jimbo la Mtwara Vijijini. Kulia ni Mgombea Uubunge Jimbo la Mtwara Vijijini, Hawa Ghasia.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269