Breaking News

Your Ad Spot

Sep 9, 2010

KAMPENI ZA JK TANGA

Mgombea Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi, Mheshimiwa Jakaya Kikwete akiwapungia mkono mamia ya wananchi waliofurika katika uwanja wa mkutano wa mjini Handeni kwa ajili ya mkutano wa kampeni tarehe8.9.2010
Mheshimiwa Jakaya Kikwete, mgombea wa Urais kupitia ccm akimtambulisha Mgombea Ubunge wa jimbo la Handeni kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi Dr.Abdallah Kigoda wakati wa mkutano wa kampeni wa chama hicho uliofanyika mjini Handeni tarehe 8.9.2010
Mheshimiwa Jakaya Kikwete, Mgombea urais kupitia Chama Cha Mapinduzi,CCM, akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Mziha kilichoko katika wilaya ya Kilindi. Rais Kikwete yupo katika kampeni kwa ajili ya uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika tarehe 31.10.2010.
Wananchi wa mji wa Songe wakiwa na shauku kubwa ya kumpa mkono mgombea urais kupitia Chama Cha Mapinduzi Mheshimiwa Jakaya Kikwete, wapigapicha nao wanaonekana wakigombea kuchukua picha za tukio hilo mara tu baada ya rais Kikwete kumaliza kuhutubia mkutano wa kampeni tarehe 8.9.2010. PICHA ZOTE NA JOHN LUKUWI

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages