Breaking News

Your Ad Spot

Sep 9, 2010

SAKATA LA NYUMBA YA URITHI DAR

Nyumba hiyo, ipo eneo la Kichanagani, Tandika wilaya ya Temeke, ambayo baada ya baba mwenye nyumba kufariki dunia walibaki wakiishi wajane wawili, ambapo mmoja kati yao alikuwa na watoto wanane, sita wa kuime na waili wa kike, na mwingine hana mtoto.
Asiye na mtoto ndiye alizusha tafrani baada ya kuamua kuuza nyumba kinyemela kwa mfanyabiashara wa Kipemba hatimaye familia iliyokuwa ikiishi humo ikatupiwa vyombo nje,leo.
VYOMBO vya familia inayoishi katika nyumba ya urithi iliyopo mtaa wa Kichangani, Temeke, Dar es Salaam, vikiwa vimetupwa nje na mnunuzi anayedaiwa kununua nyumba hiyo kinyemela.
FUNDI wa Shirika la Umeme nchini (TANESCO) akikata umeme, katika nyumba iliyopo mtaa wa Kichangani, Temeke Dar es salaam, baada ya vyombo vya familia inayoishi katika vyumba hiyo kutolewa nje kwa lazima baada ya kuuzwa kinyemela.
MKWAWA Salum, mmoja wa wa watoto wa familia ya marehemu Salum Mkwawa,akiwa amepakizwa katika gari la polisi baada ya kukamatwa na polisi baada ya kuchachamaa akipinga familia yao kutupiwa vyombo nje ya nyumba yao, kufuatia nyumba hiyo kudaiwa kuuzwa kinyemela na mama yao wa kambo, mtaa wa Kichangani, Temeke, Dar es Salaam. 

MTOTO wa mmoja wa wapangaji katika nyumba namba MTN/L/020A mtaa wa Kichanagani, Temeke Dar es Salaam, Faisal Abdallah akibeba godoro kujerejesha ndani, baada ya vyombo vya fanilia inayoishi katika nyumba hiyo, kutupwa nje , kufuatiaa kuuzwa kinyemela.
WAPANGAJI katika nyumba ya urithi iliyopo mtaa wa Kichangani, Temeke, Dar es Salaam, wakiduwaa, baada ya vyombo vya familia inayoishi katika nyumba hiyo kutupwa nje na mtu anayedaiwa kuinunua kinyemela, (Picha zote na Bashir Nkoromo).

1 comment:

  1. In This Jennifer Lopez Nip Slip Picture, You Can Clearly See Her Nipple And Jennifer Lopez Boob. [url=http://rugbylivenow.info/2011/11/23/prime-stars-whove-asked-nude/]rugbylivenow.info/2011/11/23[/url]

    ReplyDelete

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages