Breaking News

Your Ad Spot

Sep 22, 2010

JK ASTUSHWA NA KIFO CHA MZEE NATEPE

UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

Telephone: 255-22-2114512, 2116539
E-mail: press@ikulu.go.tz
Website: www.mawasilianoikulu.go.tz
Fax: 255-22-2113425
PRESIDENT’S OFFICE,
THE STATE HOUSE,
P.O. BOX 9120,
DAR ES SALAAM.
Tanzania.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais Jakaya Mrisho Kikwete ameshtushwa na kuhuzunishwa na kifo cha Meja Jenerali Abdallah Said Natepe kilichotokea leo mchana katika hospitali ya Lugalo jijini Dar-Es-Salaam

Kufuatia kifo hicho Rais amemtumia salamu za rambirambi Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kuelezea jinsi alivyoguswa na kifo hicho cha Mzee Natepe.

“Kifo kimemchukua mwanamapinduzi, mzalendo na mwanachama wetu mwaminifu katika kipindi ambacho taifa na Chama bado kinamhitaji sana, kifo kimetunyang’anya tunu wakati huu tunaoelekea Uchaguzi Mkuu, ni huzuni kubwa kwetu, ni majonzi makubwa na hatuna neno kubwa linaloweza kuelezea huzuni hii” Rais Kikwete amesema.

Rais amepokea taarifa za kifo cha Mzee Natepe leo mchana akiwa Njombe - Mkoani Iringa ambako yuko kwa ajili ya shughuli za kampeni.

Rais, kupitia kwa Katibu Mkuu wa CCM, pia ametuma salamu za rambirambi kwa familia, ndugu na jamaa wa Marehemu Natepe.

“Mzee Natepe amekua sehemu ya maisha yangu ya kisiasa, kijamii na amenipa malezi na maelekezo mengi nikiwa kama kijana wake na amekua moja ya nguzo yangu kubwa katika shughuli zangu za kisiasa na kikazi katika maeneo yote niliyotumikia nchi yangu“ amesema Rais na kuelezea kwa masikitiko huzuni aliyonayo na kuwahakikishia kuwa yuko nao katika kipindi hiki kigumu.

“Tunamshukuru mwenyezi Mungu kwa kutupa nafasi ya kuishi na Mzee Natepe na kufanya naye kazi, tunamuomba Mungu amlaze Mzee wetu mahali pema peponi na kumpa pumziko la milele, Amina”.

Rais amesema kwenye taarifa yake.

Mwisho.
Imetolewa na Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais,

Ikulu
Dar es Salaam.
22 Septemba, 2010

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages