Breaking News

Your Ad Spot

Oct 17, 2010

FATMA MAGHIMBI AITOSA CUF, AHAMIA CCM

MGOMBEA wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akimkaribisha mwanasiasa machachari wa Zanzibar na mwanachama wa CUF, Fatma Maghimbi, baada ya kutangaza kukihama chama hicho na kujiunga na CCM, katika mkutano wa kampeni za CCm leo kwenye viwanja wa Tanganyika Packers, Kawe, Dar es Salaam.
=====
Wakongwe wawili wa siasa za vyama vingi visiwani Zanzibar Mheshimiwa Fatma Maghimbi na Juma Othman Juma wamerudisha kadi zao za CUF na kuchukua za CCM leo jimboni Kawe jijini Dar es salaam na kuahidi wenzao wengi watafuata nyayo zao kutoka CUF.

Akielezea sababu zake za kurudi CCM, Juma Othman Juma amesema ameguswa kwa kazi kubwa aliyofanya Mheshimiwa Kikwete Tanzania Bara na Visiwani hususan aliporejesha amani na utulivu visiwani Unguja na Pemba kipindi cha uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

Alisema tangu historia ya vyama vingi ianze Tanzania, kila wakati wa uchaguzi wananchi wengi wa visiwa vya Unguja na Pemba hulazimika kukimbia visiwani humo kwa kuhofia hali ya kutokuwa na usalama katika kipindi hicho.

"Lakini sasa napenda kumshukuru sana Mheshimiwa Kikwete kwa kurudisha heshima ya nchi yetu duniani kwani mwaka huu wa kampeni, hakuna hata mmoja aliyehama visiwani humo kukimbia uchaguzi" alimaliza Juma Othman akishangiliwa na umati mkubwa wa wana CCM waliojitokeza kwenye mkutano huo wa kampeni.

Mama Fatma Maghimbi amewahi kuwa waziri kivuli wa Katiba na Sheria ndani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwa kama mbunge wa Chama Cha Wananchi CUF. Naye Juma Othman Juma amewahi kuwa muanzilishi wa Chama Cha Siasa visiwani kabla ya kujiunga na Chama cha Wananchi CUF.

1 comment:

  1. Nijuavyo mimi,mwana siasa makini na asiye endekeza njaa,ni vigumu sana kuama hasa kutoka vyama vya upinzani makini na kuamia ccm.yawezekana hao wameahidiwa vyeo..njaa ni kitu mbaya sana hasa kwa yule asiyeweza kuivalia kibwaya..

    ReplyDelete

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages