Breaking News

Your Ad Spot

Oct 22, 2010

PASS OUT YA MAGEREZA YAFANA LEO

MRAKIBU wa Magereza (SP), Mzee Nyamka akimuongoza Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani,Mbarak Abdulwakil, kukagua gwaride la wahitimu wa mafunzo ya Kozi ya Uongozi ngazi ya juu na Kozi ya uongozi daraja la pili, wakati wa kufunga mafunzo hayo,leo katika viwanja vya Chuo Cha Maofisa wa Magereza, Ukonga, Dar es Salaam. Jumla ya askari 305 wamehitimu mafunzo hayo. 
Maofisa waliohitimu mafunzo ya uongozi wakipiga gwaride la nguvu

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani, Mbarak Abdulwakil, akimvisha cheo Mrakibu Msaidizi(ASP) wa Jeshi la Magereza, Emmanuel Kaganda, katika sherehe ya kufunga mafunzo ya Uongozi ngazi ya Juu na uongozi daraja la pili, leo kwenye viwanja vya Chuo Cha Maofisa wa jeshi hilo, Ukonga, Dar es Salaam
Watoto wakitoa burudani katika sherehe hizo 
Kikundi cha sanaa cha Jeshi la Magereza kikitumbuiza ngoma ya asili ya Zenji

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages