WADAU zaidi ya 100 wa CUF waliotokana Pemba kuja Zanzibar kwa ajili ya mkutano wa kufunga kampeni za chama hicho wamekwama kurudi kwao baada ya kukosa meli.
Habari zilizopatikana mjini hapa, zimedai kwamba, wengine 200 waliokuwa katika msafara huo, walifanikiwa kuondoka Unguja kwenda Pemba jana, baada ya mkutano, kwa meli ya Seagul ya kukodi.
"Kiasi cha watu 300 walikuja kwa nyakati tofauti kutoka Pemba na kuhudhuria mkutano wa kufunga kampeni za CUF uliofanyika viwanja vya Maisara, juzi Jumamosi, kabla ya uchaguzi uliofanyika jana, na baada ya mkutano huo 200 waliondoka", kilisema chanzo cha habari hii.
Chanzo chetu kimedai kwamba, wafuasi hao wa CUF kutoka Pemba wengi wao walifikia maeneo ya Daraja Bovu, na kwamba wale waliokwama bado wao eneo hilo.
Katika mkutano wa kampeni wa kufunga kampeni za CUF, ulijaa maelfu ya watu, kiasi cha kusababisha viwanja vya Maisara kufurika hadi pembezoni mwa barabara.
Inadaiwa kwamba CUF ilileta watu ili kuhakikisha mkutano huo unakuwa na watu wengi kama ishara kwamba chama hicho kina wafuasi wengi ambao lazima wakiwezeshe kuibuka na ushindi baada ya uchaguzi uliofanyika leo
Wafuasi wa CUF waliohudhuria mkutano wa kufunga kampeni za chama hicho, viwanja vya Maisara, Jana, ambao inadaiwa miongoni mwao waliotoka Pemba kuja kuwapa tafu wenzao wa Unguja. na sasa inadaiwa eti baadhi yao walishindwa kurudi huko, leo
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269