Wafuasi wa CUF wakiwa kwenye Ofisi za Tume ya Uchaguzi zanzibar (ZEC) kushinikiza mgombea wa chama hicho Maalim Seif Shariff Hamad atangazwe kuwa mshindi.
==============================
Tume ya uchaguzi Zanzibar imetangaza matokeo ya kura ya Urais katika majimbo kumi na tano ambapo mgombea wa Chama cha Mapinduzi, Ali Mohamed Sheini ameibuka mshindi katika majimbo kumi na tatu.
Mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi Zanzibar- ZEC, Khatibu Mwinyichande ametangaza matokeo hayo mbele ya waandishi wa habari, ambapo amesema katika jimbo la Fuoni watu elfu 9, 367 sawa na (86.0%) kati ya wapiga kura 10,880 waliojiandikisha wamepiga kura. Dkt. Sheini amejipatia kura 6,351(61.0%) katika jimbo hilo.
Mtoni - ugunja watu 8, 768(90.7%) kati ya 9, 672 waliojindikisha wamepiga kura ambapo Dkt. Sheini amepata kura 3, 746(43%)Huko Dole kati ya watu 8, 017 waliojiandikisha ni asilimia 86.6 ya wapiga kura 6, 972 ndio wamepiga kura.Mgombea huyo wa CCM amepata kura 4, 777 sawa na asilimia 69.9%
Katika jimbo la Dimani waliojitokeza kupiga kura ni watu 11,383(88.8%) kati ya watu 12,813 waliojianikisha, Dkt. Sheini alijipatia kura 6, 225(55.5%)Kiembesamaki ni asilimia 35 nukta nne tu yaani watu 3, 856 kati ya watu 10, 884 wamejitokeza kupiga kura ambapo Dkt.Sheini amepata kura elfu 2,734 sawa na asilimia 71.8
Kwa upande wa jimbo la Mwanakerekwe ni watu elfu 7,293 sawa na asilimia 90.5 kati ya watu 8,064 waliojiandikisha kupiga kura ndio wameshiriki katika zoezi la kupiga kura. Mgombea wa CCM amekipata asilimia 60.4 yaani kura 5338. Huko Bububu Dokta Sheini amepata kura 4, 458(51.8%) kati ya kura 8,727 ya kura zilizopigwa. Watu 9,809 walijiandikisha kupiga kura katika jimbo la Bububu
Wapiga kura elfu 6,203 kati ya 7,242 waliojiandikisha kupiga kura wameshiriki katika uchaguzi ambapo Dkt.Sheini amepata asililimia 62.2 baada ya kupata kura 3,755Mfenesini Dokta Sheini amepata kura 3755 sawa na asuiimia 62.2. Wapiga kura 6203(85.75) kati ya 7242 waliojiandikisha kupiga kura wameshiriki uchaguzi huo.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa ZEC katika jimbo la Mpendae watu 8,596 sawa na asilimia 90.9 ya watu waliojiandikisha kupiga kura wameshiriki katika uchaguzi huo na Dkt. Sheini wa CCM amepata kura 4,870 ambazo ni sawa na asilimia 57.5 wakati mpinzani wake wa karibu Sharif Hamad Seif wa CUF akipata kura 3,546 sawa na asilimia 41.8.
Huko Kuhani katika wapiga kura 7,497 waliojiandikisha 6,459(86, 2%) wameshiriki kupiga kura, katika kura hizo Dkt Sheini amepata asilimia 78 .1 ya kura zilizopigwa. Katika jimbo hili Hamad amepata asilimia21.1.
Katika jimbo la mji mkongwe idadi ya waliojitokeza kupiga kura ni 6, 414 sawa na asilimia 85.6 ya watu 7, 495 waliojiandikisha, mgombea wa CCM Dkt Sheini amepata kura 1,589 sawa na asilimia 25.1. Hamad amepata kura 4, 717 sawa na asilimia 74.5.
Matokeo pia yameonyesha kuwa katika jimbo la Amani watu 6,837 (89.5%) kati ya 7,641 waliojiandikisha kupiga kura. Sheini ameibuka na kura 4, 367 sawa na asilimia 64.9 % huku Hamad akipata kura 2, 312 sawa na asilimia 34.4.
Katika jimbo la Raha Leo Dokta Sheini amepata asilimai 64.2%(4043) kati ya kura 6,399 zilizopigwa kutoka watu 7,229 waliojiandikisha kupiga kura na Hamad amepata kura 2216 (35.2%)
Kutoka Kikwajuni Sheini imejipatia kura 4,534(70.5%) kati ya kura 6,513 zilizopigwa na waliojiandilkisha ni watu 7,910 nae Hamad amepata kura 1, 860 (28.9%)
Dkt. Sheini amepata kura 2734 sawa na asilimia 71.8% ya kura 3856, nae Hamad amepata kura 1, 041(27.2%) ambapo watu 4698 walijiandikisha kupiga kura katika Jimbo la Kiembe Samaki.
Last Updated ( Monday, 01 November 2010 04:05 )
------------------------------------
Jumla ya majimbo ishirini na manne yameshaweza kutolewa matokeo ya uchaguzi wa urais wa Zanzibar Kisiwani Unguja .
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar Khatibu Mwinyichande amesema matokeo hayo ambayo yametolewa ni matokeo ya majimbo 7 ambayo yanaongeza idadi ya majimbo kufikia Ishirini na nne hadi sasa.
Katika Jimbo la Koani ,Chama cha Mapinduzi kimepata kura 7,247 huku Chama cha Wananchi CUF kikipata kura 3,099, Chama cha AFP kikipata kura tisa, Jahazi asilia kura thelathini,Tadea kikiwa na kura 18, NCCR Mageuzi kura 26 na NRA wamepata kura 21.
Jimbo la Chwaka Mkoa wa Kusini Unguja Chama cha Mapinduzi kimepata kura 7,365 huku Chama cha CUF kikipata kura 1,610, Chama cha AFP kikipata kura 36, Tadea kura 13, NCCR Mageuzi kura tisa, NRA kura Kumi na nane na Jahazi Asilia kura 33.
Na katika Jimbo la Muyuni Chama cha Mapinduzi kimepata kura 6,652, CUF kura 1,316, Chama cha AFP kura 9 , Jahazi Asilia kura 15, NCCR Mageuzi kura 4 na NRA kura 14 huku Chama cha Tadea kikipata kura 13.
Mwinyichande amesema katika Jimbo la Makunduchi , Chama cha Mapinduzi kimepata kura 6,544, huku CUF kikipata kura 1256, AFP kura 13, Jahazi Asilia kikipata kura 15, NCCR Mageuzi kura 46 na Tadea kura 5.
Jimbo la Kitope matokeo yanaonyesha Chama cha Mapinduzi kikipata kura na 5,183, Chama cha CUF kikipata kura 1,186 huku Chama cha AFP kikipata kura 13, NCCR Mageuzi kura nne, NRA kura nane na TADEA kikipata kura 14.
Aidha katika Jimbo la Bumbwini Chama cha Mapinduzi kimeongoza na kupata kura 3,362, Cuf kikipata kura 2,377 huku AFP kikipata kura 13, Jahazi Asilia kura 8, NCCR Mageuzi kura 4 na Chama cha TADEA na NRA vikipata kura 10 kila chama.
Kadhalika Jimbo la Magomeni Chama cha Mapinduzi kimeongoza kwa kura 5,200 huku Chama cha CUF kikipata kura 3,494, Jahazi Asilia kikiondoka na kura 10, NCCR Mageuzi kura 8, NRA kura 13 na TADEA kikipata kura 18
Last Updated ( Monday, 01 November 2010 14:11 )
© Michuzi
Monday, November 01, 2010
Permalink
Mtumie Rafiki Yako
Maoni 8
VIWANGO VYA MAAMBUKIZI YA SARATANI YA MATITI VYAONGEZEKA - AMI
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269