Breaking News

Your Ad Spot

Nov 3, 2010

DK SHEIN AAPISHWA

*Ampongeza Rais Kikwete kwa kuongoza maridhiano Zanzibar

JAJI Mkuu wa Zanzibar Hamid Mahamoud. akimwaapisha Dk. Ali Mohamed Shein kuwa rais wa Zanzibar, katika sherehe iliyofanyika katika Uwanja wa Amaan, mjini Zanzibar, leo. Katikati ni Rais aliyemaliza muda wake, Dk. Amani Abeid Karume. 
Dk. Shein akipigiwa mizinga 
Kisha akakagua gwaride la  Alfa, la vikosi vya Ulinzi na Usalama 
Halafu Dk. Amani Abeid Karume akamkabidhi mikoba na kumpongeza kama hivi 
Ndege maalum akipita kwenye anga ala Uwanja wa Amaani ikimwaga vipeperushi vya kumpongeza Rais wa Zanzibar, Dk. ali Mohammed Shein. 
Rais Jakaya Kikwete akimkumbatia kwa furaha ya pekee, Dk. Ali Mohamed Shein baada ya kuapishwa. Kabla ya kuwa Rais wa Zanzibar, Dk. Shein alikuwa Makamu wake wa Rais.  
Baada ya kuapishwa Dk. Sheni akasalimia viongozi mbalimbali akiwemo First Lady, Mama, Mwanamwema Shein. 
Rais Jakaya Kikwete na Rais mpya wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein wakipokea salamu za heshima za vikosi vya ulinzi na usalama 
Rais mpya wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein akihutubia wananchi baada ya kuapishwa. 
Rasi Mstaafu wa Zanzibar Amani Abeid Karume, akiingia kwa kusindikizwa na pikipiki kibao za polisi, katika uwanja wa Amaan. Baadaye pikipiki hizo zilihamia kwa Dk. Shein wakati akiondoka baada ya kuapishwa. 
Rais mstaafu wa Zanzibar, Amani  Abeid Karume, akikagua gwaride la mwisho,  muda mfupi kabla ya kumpatia mikoba ya uongozi, Dk. Shein. 
ASKARI waliokuwa wanacheza gwaride maalum katika sherehe hiyo walikabiliana na hali  ngumu ya  jua kali, Pichani, mmoja wakimtoa baada ya kuanguka. 
Watumishi wa Red Cross, wakimsaidia mtu aliyeishiwa nguvu na kuanguka, wakati shamrashamra za sherehe hizo zikipamba moto. 
Wafuasi wa CCM akishangilia jambo lililowakonga nyoyo. 
Wafuasi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na CUF wakiwa wamehudhuria katika sherehe hizo.
Aliyekuwa mgombea mwenza kwa tiketi ya CCM, Dk. Mohamed Gharib Bilal akiteta kwa chati na Waziri Mkuu mstaafu, Dk. Salim Ahmed Salim
Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye na aliyekuwa spika wa Bunge lililopita, Samwel Sitta, wakawa wanateta jambo fulani  
Kutoka Kushoto, Waziri Kiongozi mstaafu, Shamsi Vuai Nahodha, Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi na Waziri Mkuu Mizengo Peter Pinda wakiwa ndani ya nyumba 
Kutoka kushoto,  Mama Shadya Karume, Rais Mstaafu Benjamin Mkapa, Dk. Salmin Amour Jumaa a.k.a Komandoo na Naibu Waziri Kiongozi mstaafu, Ali Juma Shamhuna.
Rais Jakaya Kikwete akiondoka Uwanja wa Amaan, baada ya shughuli ya kuapishwa Dk. Shein 
Watu wakijipanga nje ya Uwanja wa Amaani kuweza kumuona Dk. Shein wakati akitoka baada ya kuapishwa
======================================

HABARI KAMILI

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi mpya, Dk. Ali Mohamed Shein amempongeza na kumwagia sifa Rais Jakaya Mrisho Kikwete kwa mchango wake mkubwa katika kuongoza na kusimamia maridhiano ya kisiasa katika Zanzibar.

Aidha, Dk. Shein amewashukuru Wazanzibari kwa kumpa heshima ya kumchagua kuweza kuwa Rais wa Saba Tanzania Visiwani.

Akiwashukuru wananchi baada ya kuwa ameapishwa kuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi leo, Jumatano, Novemba 3, 2010, kwenye Uwanja wa Amani mjini Zanzibar, Rais Shein amemwambia Rais Kikwete ambaye alikuwa miongoni mwa viongozi waliohudhuria sherehe za kuapishwa Mheshimiwa Shein.

“Mheshimiwa nakupongeza sana kwa juhudi zako kubwa za kuongoza na kuleta maridhiano ya kisiasa katika Zanzibar. Sote tunafahamu fika jitihada zako katika jambo hili.”

Maridhiano ya kisiasa katika Zanzibar yalikuwa moja ya mambo ya msingi ambayo Rais Kikwete aliahidi kuyashughulikia tokea mwanzo wa Urais wake.

Alilitaja jambo hilo miongoni mwa mambo makubwa ambayo Serikali yake ingelishughulikia wakati anazindua Bunge kwa mara ya kwanza Desemba 30, 2005, mjini Dodoma.

Rais Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi alifuatilia suala hilo kwa kuwasilisha hoja ya kuanzisha mazungumzo kati ya CCM na Chama cha Wananchi (CUF) kwenye kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa kilichofanyika Butiama, Mkoani Mara, Machi 2008.

Dk. Shein amewaambia wananchi kwenye Uwanja wa Amani kuwa washindi wa kweli wa Uchaguzi Mkuu uliofanyika Zanzibar Jumapili iliyopita ni Wazanzibari wenyewe.

“Washindi wa kweli kweli wa uchaguzi wa Jumapili iliyopita ni wananchi wenyewe wa Zanzibar. Tumefanya uchaguzi mzuri na wa amani na sasa uchaguzi umemalizika. Kazi sasa ni kujenga Zanzibar yetu na Zanzibar ni yetu sote.

Dk. Shein amemshukuru Mungu kwa kuwawezesha Wazanzibari kufanya uchaguzi salama na kwa utulivu na amekishukuru Chama cha Mapinduzi kwa kumwamini kwa kumpa nafasi ya kuwania Urais wa Zanzibar na pia kushiriki katika kumtafutia ushindi.

Mapema Dk. Shein aliapishwa kuwa Rais wa Zanzibar katika sherehe iliyohudhuriwa na maelfu kwa maelfu ya wananchi na wageni waalikwa akiwamo Mheshimiwa Amaan Abeid Karume, ambaye amemaliza kipindi chake cha Urais wa Zanzibar leo hii.

Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.

03 Novemba, 2010
=================

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages