Breaking News

Your Ad Spot

Nov 1, 2010

DR.SHEIN ATANGAZWA KUWA RAIS MTEULE WA ZANZIBAR, USIKU HUU.

Chachandu Daily ambayo imeshuhudia 'live' tukio hili la kihistoria, inakupa habari katika picha na habari kamili mwisho wa picha hizo.
Dk. Shein akiingia katika ukumbi wa Hoteli ya Bwaani kupokea matokeo


Aliyekuwa mgombea wa urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CUF, Seif Shariff Hamad ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Chama hicho, akimpongeza Rais mteukle wa Zanzibar, Dk. Ali Mohammed Sheni, baada ya matokeo kutangazwa na Tume ya Uchaguzi Zanzibar, katika ukumbi wa Hoteli ya Bwawani mjini Zanzibar  
Kisha Maali Seif akampongeza mwana-CCM wa siku nyingi aliyewahi pia kuwa waziri katika serikali ya Muungano wa Tanzania, Mzee Hassan Nasoro Moyo kwa ushindi wa Dk. Shein 
Mama Mwanamwema Shein akamkumbatia kwa furaha Mumewe, Rais Mteule wa Zanzibar, Dk. Shein baada ya kutangazwa matokeo. Kulia ni Mzee Nassoro Moyo akishuhudia 
"Hongera Mzee", akasema Mama Mwanamwema 
"Hongera Baba" akasema Binti yake, Zaina Shein 
Kijana  wake naye Amani  Sheini akafanya vivyo hivyo kwa kukmkubatia akimpongeza kwa ushindi huo 
"Hongera Kijana wangu", Mzee Nassoro Moyo akasema, wakati akimpongeza Dk. Shein baada ya kutangazwa matokeo 
Kadhalika, Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT)-Zanzibar, naye akampongeza Dk. Sheini kwa kuwa alikuwa miongoni mwa watu waliokuja naye beneti ukumbini  
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar-ZEC, Khatib Mwinchande akitangaza matokeo  
Dk. Shein , Mama Mwanamwema Shein na Mzee Nassoro Moyo wakawa wanafuatilia kwa makini wakati matokeo yakitangazwa. 
Watoto wa Dk. Shein, Amani, Zaina na Shaaban nao wakawa makini kusikiliza matokeo hayo 
Maalim Seif naye akawa makini kusikiliza wakati matokeo yakitangazwa na ZEC
=================================
Zikafuatia Shamrashamra, mitaani kukawa hapatoshi baada ya Dk. Sheni kutangazwa mshindi kwa tiketi ya CCM 
Watu akishangilia amatokeo hayo katika eneo la Kisonge ambako kuna ngome kubwa ya CCM 
Watu wakajipanga barabarani katika mitaa kadhaa kushangilia ushindi huo, huku wengine kama dada huyu wakipuliza mavuvuzela 

Vijana wakakoga katika madimwi ya maji ya mvua iliyonyesha asubuhi, kwa furaha ya Dk. Shein kushinda kwa tiketi ya CCM, hapa ni katika eneo la Raha Leo 
Wakubwa kwa watoto wakakesha wakishangilia  
Wana-CCM wakapita huku na huko kwa magari ya aina mbalimbali kushangilia
======================================
HABARI KAMILI
MWENYEKITI wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) Khatib Mwinyichande, amemtangaza Dk. Ali Mohamed Sheni kuwa rais mteule wa Zanzibar wa awamu ya saba kwa kupata asilimia 50.1 dhidi ya mpizani wake Seif Sharif Hamad aliyepata asilimia 49.1.

         Alisema Dk. Sheni alipata jumla ya kura 179,809, Seif kura 176,338, Said Soud said kura 480, Kassim Bakar Ally kura 803, Ambar Haji Khamis kura 363, Haji Khamis Haji kura 525 na Juma Ali Khatib kura 497.
         Mwinyichande alisema watu waliojiandikisha walikuwa 407,658, kura zilizopigwa zilikuwa 354,924, kura halali zilikuwa 358,815, kura zilizoharibika 6,109.
        Seif alimpongeza Dk. Sheni kwa kupata ushindi huo na alimsifu kuwa ana uwezo, uzoefu na mahaba ya kuiongoza nchi yake. Alisema ushindi wa Dk. Sheni ni uametokana na uamuzi wa wazanzibari.
       Alisema tume ya uchaguzi ya Zanzibar imefanya kazi nzuri kwakuwa uchaguzi ulikuwa haki na huru, lakini alimuomba mwenyekiti wa tume kurekebisha kasoro za baadhi ya maofisa wake wanaokiuta taratibu za uchaguzi.
       Seif alisema mwenyekiti wa tume na maofisa wake wa ngazi ya juu wanafanya kazi nzuri, lakini baadhi ya maofisa wa chini ndio wamekuwa wakileta dosari. Alimpongeza Dk. Sheni kwa kumkubatia na kumuomba awaeleze wafuasi wa CCM wasiwabeze wenzao wa CUF kwakuwa ushindi wake ni ushindi wa wazaznibari wote. Alisema uchaguzi ulikuwa huru iklinganishwa na uchaguzi uliopita.
       Kwa upande rais mteule Dk. Sheni alimsifu Seif kwa hotuba yake fupi lakini yenye maneno mazito na kwamba amemtia moyo sana katika kuwatumikia wazanzibari.
      Aliwashukuru maofisa wa tume na wazaznibar wote kwamba atafanya kwa ufasini katika kuiongoza serikali ya umoja wa kitaifa.
Chachandu Daily Blog, inampongeza Dk. Shein na Chama Cha Mapinduzi kwa jumla kwa ushindi huu

2 comments:

  1. why not...

    ReplyDelete
  2. This video post is really impressive, the echo feature and the picture feature of this tape post is genuinely amazing.

    ReplyDelete

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages