WAUMINI wakiswali katika msikiti wa Manyema, Dar es Salaam, leo
KAIMU Mufti wa Tanzania, Sheikh Ismal Habib, akitoa mawaidha wakati wa ibada ya Eid El Hajj na Baraza la Eid, leo katika Msikiti wa Simbambali wilayani Temeke jijini Dar es Salaam. Mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Rais Dk. Mohamed Gharib Bilal. (Picha na Muhidin Sufiani)
MOHAMMED Salim, akimsaidia mtoto wake Abdullatif, kuruka dimwi la maji, katika eneo la Kariakoo, wakati wakienda kusali sala ya Idd El Hajj, leo katika msikiti wa Manyema, Dar es Salaam. (Picha na Chachandu Daily)
RAIS wa Zanzibar, Alhaj Dk. Ali Mohammed Sheni, akisalimiana na Rais mstaafu wa Zanzibar, Dk. Amani Abeid Karume baada ya Baraza la Idd lililofanyika katika Jumba la Wananchi Forodhaniani mjini zanzibar, ikiwa ni shamra shamra za Sikuu ya Idd el Haj,ambapo kila mwaka waislamu Duniani kote husheheeka Sikukuu hiyo.Wapili kushoto ni makamu wa Rais wa Zanzibar, Seif Shariff Hamad. (Picha na Ikulu, Zanzibar).
MAKAMU wa Rais Dk. Mohamed Gharib Bilal, akihutubia waumini katika sala ya Eid El-Hajj na Baraza la Eid, leo kwenye Msikiti wa Simbambali Wilayani Temeke. (Picha na Muhidin Sufiani).
LIDYA akinyonyesha mtoto wake wa kike, leo katika hospitali ya Mwanayamala, Dar es Salaam, ambako alijifungua mtoto huyo usiku wa kuamkia sikukuu ya Idd El Hajj. Jumla ya watoto 9 walizaliwa katika mkesha huo watano kati yao wakiwa ni wa kiume.
WATOTO wa familia moja, Mohammed, Zera na Asha Chikawe, wakichambua mchele kwa ajili ya kupikwa pilau ya kula wakati wa sikukuu ya Idd El Hajj, leo nyumbani kwao Kawe mjini Dar es Salaam. Pilau ni chakula maarufu ambacho hupedwa kuliwa na familia nyingi nyakati za sikuu.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269