Breaking News

Your Ad Spot

Nov 16, 2010

PINDA WAZIRI MKUU; ATHIBITISHWA RASMI NA BUNGE

MBUNGE wa Katavi, Mizengo Pinda amethibitishwa na Bunge kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania, ikiwa ni awamu yake ya pili baada ya kuwa na wadhifa huo kwa miaka takriban miwili na nusu katika awamu ya kwanza ya uongozi wa Rais Jakaya Kikwete mwaka 2005.Pinda amethibitishwa rasmi baada ya jina lake kuwasilishwa kwa Spika wa Bunge, Anna Makinda jioni hii, kuwa ndilo changuo lake.Baada ya Spika Anna makinda kulitangaza jina la Pinda, wabunge walimpigia kura ambapo alipata kura 277 na za hapana 49. Kufuatia hatua hiyo, sherehe ya kuapishwa Waziri Mkuu mteule, Mizengo Pinda zitafanyika keshokutwa, katika Ikulu Ndogo ya Chamwino nje kidogo ya mji wa Dodoma, ambapo Rais Kikwete atamwapisha.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages