Breaking News

Your Ad Spot

Nov 3, 2010

JK AWAPONGEZA DK. SHEIN NA MAALIM SEIF

UNITED REPUBLIC OF TANZANIA DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

Telephone: 255-22-2114512, 2116539
E-mail: press@ikulu.go.tz
Website: www.mawasilianoikulu.go.tz

Fax: 255-22-2113425


PRESIDENT’S OFFICE,
THE STATE HOUSE,
P.O. BOX 9120,
DAR ES SALAAM.
Tanzania.


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
RAIS Jakaya Mrisho Kikwete ametuma salamu za pongezi kwa Wazanzibari pamoja na viongozi wakuu wa Tanzania Visiwani kufuatia kumalizika kwa utulivu na amani kwa Uchaguzi Mkuu, na kutangazwa kwa Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Dk. Ali Mohamed Shein, kuwa Rais Mteule.

Katika salamu hizo, Rais Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM amesema kuwa ushindi wa Dk. Shein ambao umeungwa mkono hadharani na Kiongozi wa chama cha upinzani cha CUF, Seif Shariff Hamad umefungua ukurasa mpya wa siasa za maridhiano katika Zanzibar.

“Ni siku ambayo tunafungua ukurasa mpya na kuzika rasmi siasa za uhasama katika Visiwa vya Unguja na Pemba,” amesema Rais Kikwete katika salamu za pongezi alizozituma usiku wa jana, Jumatatu, Novemba Mosi, 2010.

Rais Kikwete alituma pongezi hizo baada ya Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) kuwa imemtangaza Dk. Shein kuwa mshindi wa kura ya Urais wa Zanzibar iliyopigwa juzi, Jumapili, Oktoba 31, 2010.

Ushindi huo wa Dk. Shein wa asilimia 50.1 uliungwa mkono na Seif Shariff Hamad ambaye alimpongeza mshindi na kuahidi kufanya naye kazi kwa karibu kwa maslahi ya Wazanzibari na Visiwa vya Zanzibar.

Chini ya maridhiano kati ya CCM na CUF, Seif Shariff Hamad atakuwa Makamu wa Kwanza wa Rais katika Serikali ya Umoja wa Kitaifa itakayoundwa kufuatia uchaguzi wa juzi.

Maridhiano hayo ya Zanzibar na upigaji kura wa amani na utulivu zamu hii, tofauti na miaka ya nyuma, yametimiza ahadi aliyoitoa Rais Kikwete wakati anazindua Bunge Desemba 31, 2005, ambako aliposema kuwa ilikuwa dhamira yake kuleta utulivu wa kisiasa Tanzania Visiwani.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.

02 Novemba, 2010

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages