Breaking News

Your Ad Spot

Nov 3, 2010

DK. SHEIN KUAPISHWA LEO

RAIS mteule wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein anaapishwa leo, katika sherehe zitakazofanyika katika Uwanja wa Amani mjini Zanzibar, ambapo maelfu ya watu kushuhudia tukio hilo la kihistoria. Bila shaka Makamu wake, Katibu Mkuu wa chama cha upinzania cha CUF, Maalim Seif Shariff Hamad anatarajiwa kuhudhuria sherehe hizo. Seiff ambaye alichuana na Dk. Shein kuwania urais wa Zanzibar, atakuwa Makamu wa Rais wa zanzibar kutokana na mabadiliko ya Katiba ya nchi hiyo yaliyopitishwa na wananchi, yanayokubali kuwa Zanzibar itakuwa na serikali ya mset0. Kuapishwa kwa Dk. Shein kunafuatia kushinda kwa silimia 50.1 katika uchaguzi uliofanyika Jumapili, iliyopita ambapo Maalim Seif alipata asilimia 49.1.
Chachandu Daily, inazitakia kila la kheri sherehe hizo

1 comment:

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages