Breaking News

Your Ad Spot

Nov 14, 2010

NDUGAI AMETEULIWA NA CCM KUWANIA UNAIBU SPIKA KWA TIKETI YA CHAMA HICHO LEO

MBUNGE wa Kongwa, Job Ndugai (Pichani) amechaguliwa na CCM kugombea Unaibu Spika wa Bunge kwa kupata ushindi wa kura  197 za ndiyo  kati ya 199 zilizopigwa, huku moja ikiharibika na nyingine ikimkataa. Alipigiwa kura ya ndiyo au hapana kutokana na wagombea wawili kujitoa, hivyo kubaki pekee.


Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi, John Chiligati, alisema leo kuwa, mkutano wa Kamati ya Wabunge wa CCM imempa ushindi wa kishindo Ndugai, aliyekuwa Mwenyekiti wa Bunge lililopita.


Akizungumza na waandishi wa habari, Chiligati alisema hadi jana jioni, wanachama watatu wa CCM walijitokeza kuwania nafasi hiyo, ambao ni Ndugai, Mbunge wa Peramiho, Jenista Mhagama na Mbunge wa Magu, Dk. Festus Limbu.


Alisema wakati wa mkutano jana, Dk. Limbu alitangaza kuondoa jina lake kwenye kinyang’anyiro hicho, akisema hana sifa kama walizonazo wagombea wenzake.


Kwa mujibu wa Chiligati, Jenista, aliyekuwa Mwenyekiti wa Bunge lililopita alipokuwa akijieleza mbele ya wagombea, alisema anaondoa jina lake, hivyo asipigiwe kura.



Kwa upande wake, CHADEMA
imemteua Mbunge wake wa jimbo la  Mbulu, Mustapha Akonay, kuwania unaibu spika.

Uchaguzi wa Naibu Spika wa Bunge utafanyika Jumanne ijayo, ambapo kesho saa 10 jioni ni siku ya mwisho ya kuwasilisha majina ya wagombea wa nafasi hiyo katika Ofisi ya Bunge mjini Dodoma.

1 comment:

  1. Kwangu mimi kama spika ni chama tawala, basi naibu awe chama cha upinzani...

    ReplyDelete

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages