Kiongozi wa bendi ya DDC Mliman Park, wana Sikinde ngoma ya ukae, Habibu Mgalusi akizungumza na waandishi wa habari jinsi bendi hiyo itakavyoshiriki Tamasha hilo. Kushoto ni mwanamuziki wa bendi hiyo, Rehani Bitchuka na wengine kutoka kulia ni Wakurugenzi wa Hoteli ya Peacock, Joseph Mfugale na Damasi Mfugale
==================================
Habari Kamili
Peacock Hotel ni hoteli inayojali wateja wake kwa kiwango cha juu. Ili kudumisha na kuendeleza mila, desturi, na utamaduni wa mtanzania, hoteli ilianzisha Usiku wa Mtanzania ambapo vyakula vya asili ya Tanzania vinaandaliwa kwa ladha ya asilia. Ni hoteli pekee nchini Tanzania ambayo inadumisha menu halisi ya kitanzania.
Usiku huu unatimiza miaka kumi(10) mwaka huu tangu uanzishwe. Kila Jumatano usiku panakuwepo vyakula vya kitanzania vya aina mbalimbali na makabila mbalimbali. Mandhari ya hotel hugeuka kuwa ya asili ili kuleta maana halisi ya lengo la usiku huu.
Tarehe 3.12.2010 ni siku ya kusherehekea kutimiza miaka kumi ya Usiku wa Mtanzania katika ukumbi wa Karimjee kuanzia saa 12:00 jioni hadi saa 6:00 usiku.
Shamrashamra hizo zitapambwa na ngoma za asili pamoja na muziki kutoka kwa Kidum-Kenya, Lady Jay Dee, Sikinde-Ngoma ya Ukae, na Waane Star.
Tunapenda kutoa shukrani za dhati kwa wateja wetu wote ambao wanaendelea kuburudika kwa milo ya kitanzania pamoja na burudani za asili. Kwa kutambua uwepo wao na kuthamini usiku huu tunawaahidi huduma bora zaidi na siku ya sherehe tutawatambua rasmi baadhi yao kwa niaba yaw engine kwa kuwapa zawadi.
Washiriki wenzetu katika kuunga mkono Usiku wa Mtanzania kutimiza miaka kumi ni Benki ya Posta, Shear Illussion, Vayle Springs, na Precision Air. Hawa wanadhihirisha dhamira yao ya kuunga mkono mila na desturi za kitanzania.
Kwa maelezo zaidi wasiliana na Mr.Damas Mfugale kwa namba 0789-280112
Shikamoom mzeenapenda kukujulisha mimi nikijana mtanzania ninaeshi Washington Dc Marekani. Post uloweka midaa hii Umekosea baada ya kuweka mtanzania Umuweka Tanhania, Nilikuwa nakujulisha tu maana hata mimi inanitokezea. Na hapa huwa nachukua post kuweka kwa blog yangu http://swahilivilla.blogspot.com/ Asante mzee Nilitaka nikutwangie simu lakini hujaweka Number.
ReplyDeleteEmail tumia finya99@hotmail.com au kijiko12@hotmail.com
ReplyDeleteMarhaba!, kwanza naomba radhi kwako na kwa wengine waliosumbuliwa na kosa hilo, Nilii-post haraka kidogo kwa sababu nilikuwa nawahi mechi ya Kilimanjaro Stars na Somalia ambao wanachuana kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es salaam, kuwania ubingwa wa Kombe la Chaalenji. Asante kwa kazi nzuri ambayo umefanya kunijulisha ili niweze kusahihisha haraka. kwa kweli umetimiza jukumu lako la msingi, maana blogu hii ni yetu. namba yangu ya simu inapatikana hapo juu kwenye 'master head' karibu sana.
ReplyDelete