.

KCB YATIMIZA AHADI YA MILIONI KUMI ILIYOITOA MBELE YA JK

Dec 31, 2010

Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya KCB, Dk. Edmund Mndolwa (kushoto), akimkabidhi bango la hundi ya sh. milioni kumi, mkuu wa wilaya ya Hai, Dk. Norman Sigalla, katika hafla iliyofanyika leo makao makuu yaliyopo jengo la Harambee Plaza la Ubalozi wa Kenya hapa nchini. Katikati ni ,maofisa wa KCB,  Christina Manyenye na Ronald Kitti.
==========================================
STORI
BENKI ya KCB leo  imekabidhi Sh. milioni 10, kwa mkuu wa wilaya ya Hai, Dk. Norman Sigalla, kutekeleza ahadi iliyotolewa na benki hiyo kwa Rais Jakaya Kikwete, Julai mwaka jhuu.
KCB ilikabidhi fedha hizo kwa Sigalla, katika sherehe fupi iliyoifanyika , katika ukumbi wa ofisi za  makao makuu ya benki hiyo, katika jengo la Harambee Plaza la Ubalozi wa Kenya mjini Dar es Salaam.


 Mwenyekiti wa Bodi ya KCB Tanzania, Edmund Mndsolwa, alisema, fedha hizo zitatumika katika ujenzi wa darasa moja katika shuyle ya Sekondari Lyasikika, wilayahi Hai mkoani Kilimanjaro.


Mndolwa alisema, ahadi ya kutoa fedha hiyo, ilitolewa na KBC mbele ya Rais Jakaya Kikwete, June 18, mwaka huu, katika hafla ya chakula cha usiku iliyofanyika Ikulu Ndogo ya mjini Moshi.


Hafla hiyo ilikuwa imeandaliwa na serikali ya wilaya ya Hai na Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) kukusanya fedha kwa ajili yta kuchangia maendeleo ya elimu wilayani humo.


Katika makabidhiano hayo, Sigalla alisema, msaada huo ni muhimu sana na kuzitaka taasisi na wadau wengine kuiga mfano huo kwa ajili ya kuwezesha upatikanaji wa elimu bora nchini. Alisema, hadi sasa, wilaya ya Hai ina jumla ya shule 24 za sekondari za kidato cha sita ikiwemo ya Lyasika.


Kuhusu ushiriki zaidi za KCB katika kuboresha huduma za jamii nchini, Mndolwa alisema, huo ni mwendelezo wa misaada mbalimbali ambayo benki yake imekuwa ikitoa kwa jamii kwama hadi mwaka kwenye sekta za elimu, afya, mazingira na michezo.


Alisema, mwaka jana, KCB ilisaidia shule 14 vifaa mbalimbali vya shule na pia kujenga vyoo na visima katika baadhi ya shule ambapo jumla ya sh. milioni 40 zilitumika.


Mndolwa alisema, upande wa Afya, mwaka jana KCBC ilitumia Sh. milioni 14.5 kusaiodia hospitali ya Taifa Muhimbili (sh. milioni 10) na hospitali ya Buguruni (sh. milioni 4.5, huku matumizi mengine kwa ajili ya jamii yakiigharimu benki hiyo sh. milioni 70.


Kwa mujibu wa Mndolwa KCB ndiyo benki inayoongoza Afriuka Mashariuki kwa wingi kwa matawi na rasilimali kwa kuwa na matawi zaidi ya 200 na mashgine 400 za kutolea fedha (ATMs), mtandao wa benki hiyo ukizifikia Tanzania, Kenya, Rwanda na Sudan ya Kusini.

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ยช