MSHAMBULIAJI wa Kilimanjaro Stars, Nurudin Bakari (kushoto), akichuana na beki wa Burundi, Habarugira Paul, timu hizo zilipomenyana kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, katika mechi ya Kombe la Chalenji, leo. Stars iliibuka na ushindi wa mabao 2-0.
Msdhambuliaji wa Kilimanjaro Stars Mrisho Ngassa akimtoka beki wa Burundi katika mechi hiyo
Kipa wa akiba wa Burundi, akiwa na huzuni kwa timu yake kula kipigo cha mabao 2-0 katika mechi hiyo
Kutokana na watu kuruhusiwa kuingia bure, Uwanja wa Taifa, ulielemewa wakati wa mechi hiyo, ikalazimu polisi kuwafukuza mashabiki wengine kwa gari la maji ya kuwasha.
Mashabiki wakitimka kuongopa kumwagiwa maji ya kuwasha
Stars wakitoka Uwanjani kifua mbele kutokana na ushindi huo
Wachezaji wa Amahoro ya Burundi wakiwa wametahayari baada ya mechi
Mashabiki waliobahatika kuingia uwanjani wakishangilia ushindi
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269