Mkurugenzi wa Kampuni ya Altaf &Campany, Zulfiqal Ali , akimkabidhi Sh. 150,000 kocha wa mchezo wa ngumi, Rajabu Mhamila 'Super D' (kuhsoto), kwa ajili ya kwenda kushiriki mafunzo ya ukocha yaliyoandaliwa na Shirikisho la Ngumi za Riaa Tanzania (BFT). Mmakabidhiano hayo yalifanyika Dar es Salaam jana katikati ni Mke wa mfadhili huyo, Fatuma Zulfiqal na wenine ni wafanyakazi wa Kampuni Hiyo.
=================================================
Na Mwandishi Maalum
KOCHA wa Ngumi wa klabu ya Ashanti ambaye pia anatoa mafunzo ya kujitegemea Rajabu Mhamila 'Super D' leo amepata msaada wa Shilingi laki 1.5 zitakazomwezesha kushiriki kozi ya siku 10 ya ukocha iliyoandaliwa na Shirikisho la Ngumi za Ridhaa Tanzania (BFT).
Msaada huo ambao ni wa pili kwa kocha huyo kupewa ulitolewa na mdau wa michezo Zulfiqal Ali kumwezesha Super D kufanikisha malengo yake ya kuendeleza mchezo wa ngumi kwa vijana baada ya kushiriki kozi hiyo itakayoanza Desemba 14 hadi 24 Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza Dar es Salaam jana, wakati akimkabidhi pesa hizo Zulfiqal alisema ameamua kufanya hivyo ili kuungana na wadau wengine wa michezo ikiwemo serikali katika kuendeleza michezo.
"Michezo siku hizi hapa nchini ni ajira kwa vijana wetu na ili tuweze kufanikisha zaidi tunatakiwa kuwawezesha walimu kwanza ambao watatoa mwanga kwa wengine ndio maana nimeguswa katika hili na kusaidia.," alisema.
Hata hivyo Zulfiqal amewaomba wadau wengine kujitokeza kuungana na jamii kusaidia kukuza michezo ili kuwawezesha vijana wasio na ajira waweze kujiajili.
Naye Super D alisema anashukuru na kuahidi kuzingatia kozi hiyo siku zote ili aweze kupanua ujuzi ambao utawawezesha kuwasaidia mabondia wanaochipukia hapa nchini.
Awali kocha huyo alipewa msaada wa vifaa vya michezo vyenye thamani ya shilingi laki tatu na zaidi kwa ajili ya mazoezi ya mabondia wanaohudhuria mafunzo yanayotolewa na kocha huyo.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269