.

WAFANYAKAZI WA UHURU PUBLICATIONS LTD (UPL) NA WENZAO WA UHURU FM WATEMBELEA KAMPUNI YA GESI YA ORYX

Dec 3, 2010

Benjamin Msinge (katikati) ambaye ni Meneja wa ubora wa bidhaa wa Oryx, akitoa mafunzo ya msingi kuhusu bidhaa ya gesi isambazwayo na kampuni hiyo, kwa wafanyakazi wa UPL na Uhuru FM, kabla ya kuwatembeza katika maeneo mbalimbali ya kampuni hiyo ya Gesi
Wafanyakazi hao wakienda kwenye maeneo ambayo kuna shughuli hasa za  ujazaji kwenye mitungii na usambazaji gesi
Wafanyakazi wa UPL, na wa UHURU FM wakiwa nje ya Ofisi ya Maabara wakati wakisubiri utaratibu wa kuanza kutembelea maeneo mbalimbali ya kampuni
Meneja Mauzo wa Oryx,  Happiness Maro (kulia) akitoa maelekezo ya kiusalama baada ya kuwapatia kofia za helmet, wafanyakazi hao, muda mfupi kabla ya kuanza kutembelea maeneo mbalimbali ya kampuni.
Huyu ni mmoja wa wafanyakazi wa UPL akiwa katika helmet aliyopewa tayari kutembelea maeneo mbalimbali na wenzake katika kampuni hiyo
Benjamin Msinge (kulia) ambaye ni Meneja wa ubora wa bidhaa wa oryx, akimwelekeza jambo Menejea Rasilimali watu wa Uhuru Publications Ltd, wachapishaji wa magazeti ya Uhuru Mzalendo na Burudani, Lucas Kisasa, baada ya safari ya kutembelea kiwanda hicho kuanza rasmi.
Wafanyakazi hao wakionyeshwa mitungi ya gesi iliyo tayari kupelekwa kwa mawakala wa uuzaji au kwa wateja wa moja akwa moja.
Wakionyeshwa sehemu ya kujaza gesi kwa viwango vinavyotakiwa na salama kwenye mitungi
Mfanyakazi wa Oryx akionyesha namna na kutumia kifaa cha kurusha maji umbali mrefu hadi kwenye tenki la gesi  kwa ajili ya kukabiliana na  moto
Mmoja wa wafanyakazi wa UPL, Selina Wilson akijaribu kuitumia mashine hiyo ya kurusha maji ya kuzima moto. Wengine ni wafanyakazi wenzake na wa Uhuru F M
Wakionyeshwa sehemu ya kujaza gesi katika mitungi ya ujazo wa uzito wa aina mbalimbali
Wakionyeshwa na ofisa wa Oryx sehemu ya kujaza gesi katika mitungi
Wakionyeshwa sehemu yenye mambomba ya kupakulia gesi kutoka melini na pia mabomba kwa ajili ya maji ya kuzima moto

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ยช