CHADEMA wamefanikiwa kunyakua Umeya na Unaibu Meya wa Halmashauri ya jiji la Mwanza katika uchaguzi uliofanyika leo
Joseephat Manyerere ambaye ni Diwani wa Kata ya Nyakato, ndiye aliyechaguliwa kuwa Meya wa halmashauri ya jiji hilo baada ya kupata kura 17 na kumshinda Stanislaus Mabula wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) aliyepata kura 15.
Akitangaza matokeo baada ya madiwani kupiga kura ya siri, msimsmizi wa uchaguzi, Wilson Kabwe alisema kura zilizopigwa zilikuwa 32 na hakuna iliyoharibika hivyo kumtangaza Diwani wa Nyakato, Manyerere kuwa mshindi wa kiti cha umeya.
Kwa upande wa Naibu Meya, nafasi hiyo ilichukuliwa na diwani wa kata ya Mahina (CHADEMA) Charles Marwa baada ya kupata kura 17 na kumshinda mpinzani wake ambaye ni diwani wa kata ya Mirongo (CUF) Daud Mkama aliyepata kura 15.
Maeneo ya ofisi za halmashauri ya jiji hilo jana yalikuwa na ulinzi mkali wa Askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) huku wakiwa kwenye magari mawili aina ya ‘defender’.
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya uchaguzi huo, Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe alisema viongozi hao wa chama chake, watafuata kanuni na sheria na katika kuwatumikia wananchi wa jiji hilo .
Uchaguzi huo uliofanyika kwa kura za siri, awali ulifanyika Desemba 17, mwaka jana na kuahirishwa baada ya wabunge na madiwani wa Chadema kugomea kupiga kura za siri huku wabunge na madiwani wa CCM wakiafiki kura hizo hivyo kuahirishwa.
Your Ad Spot
Jan 6, 2011
Home
Unlabelled
CHADEMA WANYAKUA UMEYA/UNAUBU MEYA JIJI LA MWANZA
CHADEMA WANYAKUA UMEYA/UNAUBU MEYA JIJI LA MWANZA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269