Mgambo wakibeba vyumba kutayarisha eneo walilodhani Naibu Waziri wa Biashara na Masoko, Lazaro Nyalandu atapita, alipofanya ziara yake leo Soko Kuu la Kariakoo jijini Dar es Salaam
VIjana ambao hufanya biashara za hapa na pale nje ya soko kuu la Kariakoo, wakitiwa kashi-kash na polisi muda mfupi kabla ya kufika Nyakalandu eneo la Soko Kuu la kariakoo kufanya ziara hiyo
Lakini mlemavu huyo ambaye ni ombaomba alibahatika kubaki langoni mwa jengo la Soko hilo, bila shaka alidhani itakuwa siku njema kwake kwa Mheshimiwa Naibu waziri kupita karibu yake. Kweli alipita karibu yake kama hivi lakini akawa bize na ziara yake bila kumtupia chochote mlemavu huyo, labda hakumuona!
Halafu Nyalandu akatoa lake la moyoni lililonfanya kufanya ziara hiyo. Akasema, "kuanzia leo natoa siku 30, wafanyabiashara wote wa kigeni ambao wanajishughulisha na biashara zile zinazoziba fursa za Watanzania waondoke, la sivyo baada ya muda huo watakiona", Haiwezekani mtu anaingia nchini kama mwekezaji au analetwa na mtu mwenye kibali cha uwekezaji kama mtaalam wake, halafu mtu huyo anauza maua na bidhaa ndogondogo mitaani, hili halikubaliki" alisema.
Halafu akaondoka zake eneo hilo kwa kuwapungia mkono wadau
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269