Breaking News

Your Ad Spot

Jan 9, 2011

MAZOEZI YA MASHINDANO KUSAKA VIPAJI VY A WAIMBAJI MUZIKI WA DANSI YAANZA LEO

Mkurugenzi wa kampuni ya Makukwe Entertainment, Suleiman Mathew akitangaza kuanza kwa mazoezi ya washiriki wa shindano hilo, leo katika ukumbi wa News Msasani Beach, Dar es Salaam. 
Mathew, Karola Kinasha na Abdul Salvadol wakifuatilia mazoezi ya washiriki yalivyokuwa yakiendelea 
Moja ya makundi yatakayoshiriki maoshindano hayo, Kipepeo Group, wakifanya mazoezi.  
Mmoja wa maofisa wa kampuni ya Makukwe Entertainment, Asha, akifuatilia mazoezi hayo 
Hailat wa  Makukwe akifuatilia mazoezi hayo. Mashindano yanatarajiwa kuanza hivi karibuni

STORI
JUMLA ya washiriki 40 wameingia kambini kuanza rasmi mazoezi kujifua kwa ajili ya shindano la kusaka vipaji vya uimbaji wa muziki wa dansi linalotarajiwa kufanyika hivi karibuni.
Akizungumza na waandishi wa habari, jana, mjini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Kampuni ya Makukwe Entertainment inayoratibu shindano hilo, Suleiman Mathew, alisema washiriki hao 40, wapo katika makundi manane yenye wasanii watano kila kundi.
         Mathew alisema, kuanzia juzi washiriki hao wameanza mazoezi ya nguvu, ambapo kila kundi linachagua nyimbo linazopenda kuzifanyia mazoezi ya kuziimba huku likipigiwa vyombo vya wimbo husika na wapigaji maalum ambao watapigia kila kundi.
      Alisema, Januari 14, mwaka, maonyesho ya vikundi vyote vinavyoshiriki yataonyeshwa moja kwa moja katika kituo cha
Televisheni cha Chanel Ten, kuanzia saa 3 usiku na kurudiwa tena kesho yake kuanzia saa 8 mchana.
      Alisema, majaji katrika shindano hilo ni wanamauziki wa siku nyingi na wakongwe katika fani hiyo, Kina Tshimanga Assossa, Nyota Waziri, Ally Chocky, Abdul Salvadol na Kalora Kinasha.
      Mathew alisema kupata mshindi mashabiki watapiga kura kupitia simu zao, katika utaratibu utakaotangazwa baadaye, na kwamba mshindi atapata zawadi nono ambayo hata hivyo alisema nayo itatangazwa baadaye.
       Alisema, makundi yaliyoingia kambini, yalipatikana baada ya mchakato, uliofanyika mjini Dar es Salaam, Januari 2, mwaka huu, ambapo mchuano ulikuwa mkali hadi kupatikana hao.
      Mathew alisema, nia ya shindano hilo, ni kuinua vipaji vya wasanii wa uimbaji wa muziki wa dansi na kuinua soko na hadi ya muziki huo kwa jumla hapa nchini.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages