AKLIYEKUWAmpi gita zito la bass wa DDC Mlimani Park Orchestra,Mustafa Ngosha
(pichani) ambaye alijulikana zaidi kwa jina la Ngosha amefariki dunia ljana baada ya kusumbuliwa na maradhi kwa muda kidogo.
Ngosha alijiunga na DDC Mlimani Park miaka ya mwanzoni ya 90, akiwa anajulikana kama Charles John Ngosha ila baadae alibadili dini na Kuwa muislam na kupewa jina la Mustafa.
Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Amana,Ilala jijini Dar es Salaam,
Msiba upo nyumbani kwa marehemu pale Tandale kwa Popobawa na kwa mujibu wa mmoja wa
wanakamati ya mazishi na mwanamuziki mkongwe Hassan Rehani Bitchuka, taratibu za mazishi zinafanyika kwa ajili ya mazishi hayo kufanyika leo. Ngosha aliyezaliwa mwaka 1965, ameacha mjane na watoto kumi
Twamuombea mungu ailaze roho ya marehemu pema peponi na pole kwa wafiwa wote, kwani yote ni mapenzi yake Rabana
ReplyDelete