Breaking News

Your Ad Spot

Jan 22, 2011

SHUJAA WA SAFARI LAGER APATIKANA KUTOKA SINZA KWA WAJANJA

PAUL Luvinga,  mkazi wa Sinza E, kwa wajanja jijini  Dar es Salaam, ameibuka mshindi wa tuzo ya 'Shujaa wa Safari Lager' na kuondoka na kitita cha sh. milioni 7.

Mbali na kitita hicho, bia ya Safari Lager imetoa pia sh. milioni 3 kwa ajili ya mradi wa kijamii eneo anakoishi.

Luvinga, alitangazwa kutwaa ushindi huo, na Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Dk.  Makongoro Mahanga, katika katika hafla ya kuwazawadia washindi wa tuzo hiyo, katika ukumbi wa hotel ya City Paradise, iliyopo katika jengo la Benjamin William Mkapa, jijini Dar es Salaam, jana.


Mercy Shayo mkazi wa Bomang'ombe mkoani Kilimanjaro na Leonard Mtepa wa Mwananyamala A, Dar es Salaam, ambao waliingia na Luvinga katika fainali ya shindano hilo nao walizawadiwa sh. milioni moja kila mmoja.


Hadi matokeo yanatangazwa wote watatu walioingia fainali walikuwa ukumbini wakiwa hawajui nani mshindi kati yao, kabla ya Dk. Mahanga kufungua bahasha maalum na kumtangaza Luvinga kuwa ameibuka mshindi kwa kupata kura 1555 katika jumla ya kura 1855.

Mercy aliyepata kura 605, aliingia fainali kwa sifa za kusaidia watoto waishio katika mazingira magumu na kikundi cha kina mama waishio na virusi vya ukimwi wakati, Mtepa ambaye naye alipata kura 135, alimsaidia mjane asidhulumiwe nyumba kwa kumuongoza katika vyombo vya sheria hadi kupata haki yake huku Luvinga akitamba kwa sifa ya kuanzisha maktaba ya mtaani yake iitwayo 'Udzungwa Street Library' inayoendelea kusaidia watu wa rika zote kujisomea bure.

Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bila yake ya Safari lager, ilianza mchakato wa kumpata Shujaa huyo Novemba 24, mwaka jana, kwa lengo la kuweza kutambua juhudi za watu katika jamii ambao wamekuwa wakijitolea kusaidia makundi yenye uhitaji bila kusukumwa na vyeo au fedha walizo nazo.

Baadaye mchakato huo uliendelea kwa wananchi kutuma majina ya wale ambao walidhani wanafaa kuingia kwenye kinyang'anyiro, ambapo baadaye waliingia fainali hao watatu ambao nao walipigiwa kura kwa njia ya ujumbe mfupi wa maneno kupitia simu.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages