Breaking News

Your Ad Spot

Feb 20, 2011

MAENDELEO ENDELEVU

Dkt. Islam S. Salim,Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar akizungumza katika Mkutano wa 49 wa Kamisheni ya Umoja wa Mataifa kuhusu Maendeleo Endelevu (CSD). Akichangia mjadala kuhusu maendeleo endelevu na uondoaji wa umaskini, Dkt. Islam Salim aliyeongoza Ujumbe wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika mkutano huo, Pamoja na mengine alisisitiza uwekezaji katika miundombinu kama moja ya njia ya kuwasaidia wananchi kuondokana na umaskini hasa wale wa vijijini.



Aidha amesema pamoja na nchi zinazoendelea kujitahidi sana katika kuwaletea maendeleo wananchi wake, pamoja na kutambua hali ngumu ya uchumi inayoendelea dunia kote hivi sasa, amesisitiza haja na umuhimu wa nchi tajiri na zilizoendelea kutimiza ahadi zake za utoaji wa misaada ya kiuchumi kwa nchi maskini.


Pamoja naye wengine walioshiriki katika mkutano huo wa wiki mbili ambao umemalizika siku ya ijumaa , Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa na kupitisha maazimio mbalimbali ni Bw. Ali Khamis Juma, Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Kazi Serikali ya Mapinduzi Zanzibar aliyekaa nyuma ya Dkt. Salim, na Bi Halima. M.S. Abdalllah hayuko pichani, ambaye ni Mkurugezi wa Idara ya Ustawi wa Jamii, Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Vijana, Wanawake na Watoto ( Zanzibar).

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages