Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Mahadhi Juma Maalim (MB) akizungumza wakati wa Kongamano ambalo ni moja ya maandalizi ya Mkutano wa Nne wa Nchi 48 Maskini Zaidi Duniani mkutano huo utafanyika mwezi Mei huko Uturuki.Kongamano hilo limefanyika New Delhi, India, na kuwashirikisha Mawaziri ama Manaibu waziri kutoka nchi 32 kati ya 48. Serikali ya India kupitia Kongamano hilo imeahidi kuongeza misaada yake kwa nchi maskini zaidi ili kuzichagiza ziweze kuhitimu na kuondokana na umaskini.
Ujumbe wa Tanzania katika Kongamano hilo. kutoka kushoto ni Balozi wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Ombeni Sefue, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Mahadhi Juma Maalim na Bw. Katinda E. Kamando, Mkurugenzi wa Sera na Mipango, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269