Breaking News

Your Ad Spot

Feb 20, 2011

MABOMU GONGO LA MBOTO, MAREHEMU WA FAMILIA MOJA KUZIKWA KESHO RORYA, WAAGWA LEO DAR

MAJENEZA yenye miili ya mama na watoto wake wawili kutoka familia moja ya Jacob Nyajengo wa Mzambarauni, waliokufa kwa kuangukiwa na nyumba ya jirani, kutokana mabomu yaliyolipuka kutoka ghala la Silaha katika kambi ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Gongo la Mboto,Dar es Salaam, yakiwa nje nyumbani kwa Nyajengo, wakati wa kutoa heshima za mwisho, kabla ya kusafirishwa leo, kwenda Rorya kwa mazishi. Kushoto ni Mbunge wa Segerea, Dk. Makongo Mahanga, aliyewakilisha serikali katika shughuli hiyo ya kuaga. Picha zote na Chachandudaily.blogspot.com
Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Willibrod Slaa akiwa na My wife wake kwenye msiba huo.Alifuatana pia na wabunge kadhaa kwa tiketi ya chama hicho.
Dk. Slaa na mkewe wakitoa heshima za mwisho kwa miili ya marehemu hao

Mmoja wa waombolezaji akimfariji Nyajiego aliyekuwa mume na baba wa watoto waliofariki

Waombolezaji wakitoa heshima za mwisho kwa miili ya marehemu hao
Mzee Nyajiego (kushoto) akitoa heshima za mwisho kwa mkewe na watoto wake, kabla ya safari ya kwenda kuwazika Rorya.
Chachandudaily Blog, inatoa pole za dhati kwa Mzee Nyajiego na familia yake, kwa msiba huo

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages