Breaking News

Your Ad Spot

Feb 7, 2011

MSHINDI WA KWANZA MASHINDANO YA 'SAFARI LAGER' NYAMACHOMA KUONDOKA NA MILIONI MOJA MWAKA HUU

KAMPUNI ya Bia Tanzania (TBL) kupitia Bia yake ya Safari Lager imetangaza kuanza kwa mashindano ya Nyama Choma, na kuahidi kutoa zawadi ya kitita cha sh. milioni moja kwa mshindi wa kwanza.
      Akitangaza kuaza kwa shindano hilo ambalo mwaka huu, Meneja wa Bia ya Safari Lager, Fimbo Butala, alisema, leo kwamba mshindi wa pili atajipatia sh. 800,000, watatu Sh. 600,000, wanne sh. 400,000 na watano sh. 200,000.
      Butala (kushoto Pichani akiwa na Jaji Mkuu wa Shindano hilo, Lawrence Salvi -kulia), alisema, mchakato wa mashindano hayo, umeanza arasmi jana, na zitaendelea hatua mbalimbali hadi Machi 27,mwaka huu, itakapofanyika fainali na kwamba mwaka huu yatafanyika katika mikoa ya Dar es Salaam, Kilimanjaro, Arusha, na mkoa wa Mbeya ambao mwaka jana haukuhusishwa.
         Alisema, alitaja tofauti nyingine katika mashindano ya mwaka huu, kuwa utaratubu wa kuingiza baa kumi bora katika hatua ya awali umeachwa, badala yake sasa ni baa tano tu katika kila mkoa zitakazoingia fainali na kila mkoa utakuwa na mshindi wake.
        Butala alisema baa tano bora zitachaguliwa na wadau kwa njia ya simu ambapo wataandika neno Safari, mkoa kisha jina la baa anayopendekeza, halafu atatuma kwa njia ya ujumbe wa maneno mafupi kwenda namba 15540.
        Alisema vigezo vitakavyotanzamwa kwenye shindano hilo, ni usafi wa eneo, v ifaa na mhusika, uchaguzi na maandalizi ya nyama, jinsi ya uchomaji, muda unaotumika na jinsi nyama inavyofikishwa kwa mlaji na akwamba baa zitakazoingia fainali wahusika wake watapewa semina elekezi kuhusu vigezo hivyo

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages