Breaking News

Your Ad Spot

Feb 7, 2011

UDSM KWAWAKA, MABOMU YA MACHOZI YARINDIMA

Wanafunzi wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, wakimsubiri kwa mabango kama hili, Waziri wa Elimu, Dk. Shukuru Kawambwa, kabla ya kufika chuoni hapo kuwasili kwa lengo la kuzungumza nao kuhusu nyongeza ya sh. 10,000 wanayotaka waongezwe kwenye fedha za kujikimu. 
Mwanafunzi na bango la kuomba 10,000.
Mwanafunzi akiwa amejifunga utepe wa polisi baada ya kuung'oa eneo ulikokuwa umewekwa na polisi kwa ajili ya usalama. 
wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, wakimsubiri Waziri wa Elimu Dk. Shukuru Kawambwa kuzungumza nao. 


RICHARD Mwita, mmoja wa wanafunzi akihamasiha wenzake kuhakikisha akifika Dk. Kawambwa anatoa tamko tu la nyongeza ya sh. 10,000 la sivyo hapatoshi 
Waziri wa Elimu, Dk. Shukuru Kawambwa akisindikizwa na pikipiki ya Polisi kuingia kwenye mkutano na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, leo 
WAZIRI wa Elimu Dk. Shukuru Kawambwa na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa, Rwekaza Mukandara, wakiingia kwenye mkutano huo. 
WAZIRI wa Elimu Dk. Shukuru Kawambwa akizungumza na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, baada ya kuanza mgomo wao jana. Kushoto ni Makamu Mkuu wa chuo hicho, profesa Rukaza Mukandara. 
Kisha waziri kawambwa na msafara wake wakaondoka 
Baada ya waziri kuondoka  ndipo likazuka sheshe, polisi wakaamua kulipua mabomu ya kutoa machozi, baada ya baadhi ya wanafunzi kuwatupia chupa za maji na mawe polisi hao. 
Kama ambavyo ni kawaida kwamba inapotokea vurugu mwadhirika wa kwanza ni mwanamke  na watoto, Mambo yakawa mazito kwa mwanafunzi huyo, akaangua kilio baada ya tafrani ya mabomu 
Hawa nao wakajificha mtaroni kunusuru maisha yao 
Hawa wakakumbatiana kusubiri litakalokuwa na liwe 
Waanafunzi wakimsaidia mwenzao ambaye aliumia katika mshike mshike huo.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages