Breaking News

Your Ad Spot

Feb 16, 2011

SIMBA YAKWAA KISIKI KWA TOTO AFRICANS, AZAM FC YAPAA

TOTO Africa imeikomalia Simba na kutoka nayo 2-2 katika mechi ya mzunguko wa pili ya Ligi Kuu ya Vodacom iliyomalizika hivi punde kwenye Uwanja wa Kirumba mjini Mwanza. Simba imeshindwa kuvuka kutokana na bao la pili na la kusawazisha lililofungwa katika dakika ya 90 na mshambuliaji wa Toto, Mohammed Sudi.

   Nayo Azam FC, ikipeta baada ya kuifunga 3-0 African Lyon FC, katika mechi ya mzunguko wa pili wa Ligi hiyo, ambayo pia imemalizika mida mida hii kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
  Pichani, Mshambuliaji wa Azam, Mrisho Ngassa akishangilia, baada ya kupachika bao la kwanza dhidi ya African Lyon FC.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages