BONDIA wa Zamani na Kocha wa Ngumi wa Klabu ya ngumi ya Ashanti, Rajabu Mhamila 'Super D' yupo mbioni kutoa Video itwayo 'Super D Boxing Coach' inayozungumzia maisha yake ya mchezo huo.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Super D alisema video hiyo itakuwa sokoni muda wowote kuanzia sasa ikizungumzia maisha yake tangu alipoanza kucheza mchezo huo mwaka 1984 hadi sasa.
Aliisema Video hiyo itaonesha mapambano mbalimbali aliyocheza na dhidi ya mabondia Mbwana Matumla, Rashidi Ali na Ajibu Salumu.
Alisema lengo la kuandaa video ni kutaka kutimiza malengo yake ya kuendeleza mchezo wa ngumi kwa kuwapatia vijana nafasi ya kujifunza kupitia kwake.
Alisema kutokana na nchi ya Tanzania kuwana vipaji vingi atashindwa kuwafikia kila mmoja wao na badala yake amewapa fursa ya kujifunza kwa kuangalia video.
Alisema Video katika kuhaikisha Video hiyo inafanya vizuri sokoni ameongezea vionjo vingine kutoka kwa mabondia maarufu duniani kama Mike Tyson, Michael Mo, Junior Myweather, Mohamed Ally, Man Paqyao na Joe Fleizer.
Your Ad Spot
Feb 5, 2011
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
Kazi nzuri, tuna hamu ya kuiona video hiyo!
ReplyDelete