Breaking News

Your Ad Spot

Feb 4, 2011

WATAKA KUMUUA CHIZI KWA KUMTUHUMU UCHAWI

MTU mmoja anayedaiwa kuwa mgonjwa wa akili amenusurika kuuawa na wananchi  wa eneo la Nyasura, katika mji mdogo wa Bunda, mkoani Mara, kwa kumtuhumu kuwa ni mchawi baada ya kumkuta akiwa uchi kwenye paa la nyumba ya mkazi  wa eneo hilo.

Jeshi la polisi wilayani Bnda, limethibtisha kutokea kwa tukio hilo, juzi, saa 3:00 asubuhi, katika eneo hilo la Nyasura katika mamlaka ya mji mdogo wa Bunda.


Ofisa mtendaji wa Nyasura Thomas Bure, amemtaja mwanaume huyo kuwa Makoko Adonius (30), mkazi wa mtaa huo, na kwamba baada ya wananchi kumkuta amepanda juu ya bati akiwa uchi, walimtuhumu kuwa ni mchawi, ambapo ilipigwa yowe na wananchi kufurika eneo la tukio na silaha mbalimbali za jadi na kutaka
kumshambulia.


Bure alisema kuwa baada ya wananchi kupiga yowe, mwanaume huyo alitoboa bati la yumba hiyo kwa kutumia mikono yake na kutumbukia ndani ya nyumba hiyo, na kwamba hali hiyo iliongeza hasira kwa wananchi hao, kuwa uhenda ni mchawi na kutaka kubomoa nyumba hiyo.

Alisema kuwa mwanaume huyo alinusurika kifo, baada ya polisi kuwahi kufika katika eneo la tukio na kuwatawanya wananchi na kisha kumchukuwa na kumpeleka katika hospitali teule ya wilaya ya Bunda, ambako imethibishwa kwamba ni mgonjwa wa akili.

Mapema akizungumza na polisi katika eneo la tukio, baba mkubwa wa mwanaume huyo, Lucas Mlagara, alisema kuwa mtoto wao ni mgonjwa wa akili na si mchawi kama inavyodhaniwa, na kwamba siku hiyo mwenye nyumba ambaye ni ndugu yao hakuwepo nyumbani hapo.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages