Breaking News

Your Ad Spot

Mar 14, 2011

MTALIANO AZISAIDIA SHULE MBILI MSAADA WA VITABU VYA MILIONI 14.2

RAIA wa Italia anayeishi hapa nchini, Giseppe Tuzzeo (wanne kulia) akikabidhi Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Dar es Salaam, Yusuf Mwenda, msaada wa vitabu  vya Kiswahili, Hisabati, Sayansi na Teknohama vyenye thamani ya Sh. Milioni 14.2, kwa ajili ya wanafunzi wa madarasa ya kwanza hadi la saba katika shule za msingi Mweni na Kiumbageni, katika sherehe iliyofanyika juzi katika shule ya Mbweni. Vitabu hivyo ambavyo  Tuzzeo amevipata kwa kushirikiana na marafiki zake katika Ushirika wa Piccoli scalzi (Mtoto bila viatu), Utawezesha kitabu kimoja cha kila somo kutumiwa na watoto wawili katika shule hizo kwa madarasa yote, hali ambayo haijafikiwa katika shule nyingine zote katika Manispaa ya Kinondoni. Wapili kulia ni Naibu Meya wa Manispaa hiyo, Songoro Mnyonge

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages