Breaking News

Your Ad Spot

Mar 14, 2011

MSHINDI KILI TAIFA CUP MWAKA HUU KUONDOKA NA MILIONI 40, MICHUANO KUANZA MEI 7.

Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Angetile Osiah akizungumza wakati wa uzinduzi wa michuano ya Kili Taifa Cup, leo, katika ukumbi wa Safari Pub, ndani ya kiwanda cha Bia Tanzania (TBL) Ilala mjini Dar es Salaam. Kulia ni Meneja wa Bia ya Kilimanjaro, George Kavishe.
Kavishe na Osiah wapongezana baada ya kuzindua rasmi michuano hiyo
STORI
TIMU itakayoibuka mshindi wa kwanza katika Michuano ya Kilimanjaro Taifa Cup, yaani Kombe la Taifa, mwaka huu atacheka zaidi kufuatia wadhamini wa kichuano hiyo Kampuni ya Bia Tanzania kupitia bia yake ya Kilimanjaro Premium Lager, kuongeza dau kwa mshindi huyo ambalo ni kubwa kuliko la mwaka jana.

Akitangaza uthamini wa michuano hiyo, itakayoanza Mei 7, Meneja wa bila ya Kilimanajro, George Kavishe, leo amesema,  mshindi wa kwanza ataruka na kitita cha Milioni 40 badala ya Sh. Milioni 35 alizopata mshindi wa kwaanza mwaka jana.

Katika ukumbi wa  Safari Pub, uliopo katika Kiwanda cha Bia Tanzania (TBL), Ilala jijini i Dar es Salaam, Kabishe amesema, mbali  ya  dau la mshindi wa kwanza kupanda pia gharama za maandalizi zimetoka milioni 770 za mwaka jana, hadi kufikia sh. Milioni 800, kwa lengo la kuboresha zaidi mashindano hayo.

Kavishe alisema, dau la mshindi wa kwanza limepandishwa ili kutoa ushindani zaidi kwa timu shiriki kila moja kutamani kuwa mshindi wa kwanza, tofauti na mwaka jana au mashindano mengine yaliyopita ambapo zawadi ya mshindi wa pili ilikuwa haipishani sana na ya mshindi wa kwanza.

Alisema zawadi kwa mshindi wa pili na watatu zitabaki katika viwango vile vile vya sh. Milioni 20 kwa mshindi wa pili na milioni 10 mshindi wa tatu, viwango ambavyo alisema bado pia vinavutia ushindani zaidi.

Kavishe alitaja zawadi zingine ni mfungaji bora kupata sh. Milioni 2.5, kipa bora, kocha bora, mwamuzi bora na mcheaji mwenye nidhamu wakitengewa zawadi ya sh. Milioni 2 kila mmoja na sh. 100,000 kwa mchezaji bora atakayetangazwa baada ya kila mechi.

Akizungumzia mfumo wa mashindano ya mwaka huu ambayo ni ya nne tangu yaanze kuthaminiwa na TBL kupitia bia ya Kilimanjaro, Mkurugenzi wa Ufundi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Sadi Kawemba, alisema zinatarajiwa kushiriki timu kutoka mikoa 23 mwanachama wa TFF na timu ya taifa ya Vijana chini ya miaka 20 (U20) ambayo ilianza kuhsiriki mashindano hayo mwaka jana.

Alisema, mwaka huukutakuwa na vituo sita ambavyo kila kituo kitakuwa na timu nne vitakavyotoa mshindi wa kwanza atakayeambata na timu bora mbili kutoka kituo husika kwa ajili ya kuingia robo fainali.

Kawemba alisema, vituo ambavyo vimepangiwa kurindima michuano hiyo, lakini havijathibitishwa rasmi ni, Dar es Salaam, Dodoma, Moshi, Mwanza, Mbeya na Lindi.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah, alieleza kufurahishwa kwake na mchango mkubwa ambao umekuwa ukitolewa na TBL kupitia bia yake ya Kilimanjaro, katika kusaidia kuinua kiwango cha soka hapa nchini.

Alizitaka timu zinazoshiriki Ligi Kuu, kuitumia fursa hiyo kutafuta wachezaji bora wa kusajili katika timu zao, na kufafanua kwamba, michuano hiyo si chanzo cha kupata wachezaji wa timu ya Taifa, kama inavyodhaniwa bali wachezaji wa timu ya taifa hupatikana katika vilabu vya Ligi kuu.
Katika michuano ya mwaka jana, timu ya mkoa wa Singida, ndiyo iliibuka mshindi, baada ya kutinga katika fainali na timu ya Lindi.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages