Kimini alichovaa trafiki wa kike ambaye jina lake halikupatikana mara moja, kinadaiwa kuzua balaa huku wahuni wakimpigia miluzi.
Tukio
hilo lililojaza kadamnasi na kushuhudiwa na ‘shushushu’ wetu lilijiri
wiki iliyopita maeneo ya Mwenge jijini Dar, majira ya asubuhi.Bila kujua
‘amefotolewa’ trafiki huyo alikuwa amesimama pembeni akimtazama
mwenzake wa kiume aliyekuwa akiongoza magari huku kimini chake cha sare
ya kazi kikiwa kimepanda juu na kuonesha sehemu ya upaja wake wa haja.
“Jamani
mbona majanga? Waone wahuni wanavyokitolea macho kimini cha trafiki na
hapo amesimama. Akiinama kidogo tu mambo yote hadharani,” alisema mama
aliyekuwa akiwashangaa raia walioacha kazi zao na kujadili kivazi hicho
cha trafiki huyo.
“Tunachojua
ni kwamba hizi sare huwa wanashonewa na serikali siyo kwamba wanashona
wenyewe. Kazi yao inahitaji kufuata maadili kwa kuwa ni watumishi wa
umma. “Itakuwa ameongezeka mwili kwa sababu mbali na kuwa kifupi pia
kinambana kama kile cha trafiki mrembo wa nchini Kenya aliyeibua gumzo
mwaka jana.
“Au
inawezekana washonaji hawakumpima vizuri kwa sababu sketi zao
zinatakiwa zifike chini ya magoti,” alisema jamaa mmoja aliyekuwa
akijaribu kutafuta majibu ya kimini hicho.
Ili
kupata mzani wa habari hiyo kuhusu mavazi ya trafiki wa kike hasa urefu
wa sketi za trafiki wa kike, gazeti hili lilimtafuta Kamanda wa Kikosi
cha Usalama Barabarani, Mohammed Mpinga lakini alipopigiwa simu, iliita
mara kadhaa pasipo kupokelewa.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269