Jeshi la polisi mkoa wa Geita limewakamata waganga wa kienyeji 32 wanaopiga ramli chonganishi katika msako uliofanywa hivi karibuni ili kuhakikisha mauaji ya vikongwe na watu wenye ulemavu wa ngozi yanakomeshwa kabisa.
Akizunguza
na waandishi wa habari baada ya kufanya msako na kuwakamata waganga hao
kamanda wa polisi mkoa wa Geita Sacp Joseph Konyo amesema wakati sasa
umefika wa kuhakikisha mauaji yanayotokana na imani potofu za
kishirikina yanakomeshwa na ili kuyakomesha watu wa kwanza kudhibitiwa
ni waganga wa kienyeji wanaofanya shughuli zao pasipo kuzingatia sheria
na taratibu zilizowekwa na nchi.
Kamanda
Konyo amesema upo ushahidi wa wazi unaonyesha mahusiano ya karibu ya
mauaji haya ya vikongwe na watu wenye ulemavu wa ngozi na waganga wa
kienyeji kwani ndio wahusika wanaoagiza viungo vya Albino na ndio hao
wanaopiga ramli za uongo kuonyesha kuwa vikongwe hasa wanawake ndio
wachawi.
Kamanda
Konyo amesema serikali haiwezi kuvumilia waganga wa namna hii
wanaoipotosha jamii hivyo msako huu utaendeshwa katika mikoa yote
Tanzania bara ili kubaki na jamii salama isiyokuwa na vitisho vya mauaji
ya kikatili kama haya.
Baadhi
ya wananchi mkoa wa Geita wameipongeza hatua ya serikali kuanza sasa
kuwachukulia hatua watuhumiwa wote wanaopatikana na tuhuma za mauaji
yanayotokana na mila potofu na ushirikina.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269