.

MICHUANO KUSAKA BINGWA WA DARTS AFRIKA MASHARIKI KUANZA KESHO JIJINI DAR ES SALAAM

Apr 22, 2011

David Msambi akizungumza aleo


ZAIDI ya wachezaji 300 wa mchezo wa Darts watachuana vikali, katika michuano ya kusaka bingwa wa Afrika Mashariki wa mchezo huo,
itakayoanza kesho mjini Dar es Salaam.


Wachezaji hao wanaounda timu za taifa za nchi za Tanzania, Kenya na Uganda, Rwanda na Burundi wanatoka katika timu za vilabu vya mchezo huo katika nchi husika.


Makamu Mwenyekiti wa Darts Tanzania, David Msambi amesema leo kwamba, wachezaji wa timu za Taifa za Kenya na Uganda wameshawasili na walikuwa bado wanasubiriwa wale wa kutoka Burundi na Rwanda.


Alisema, michuano hiyo amabayo itamalizika Jumapili ii,inakusudia kumpata bingwa mpya badala ya Kenya inayoshikilia ubingwa huo baada ya kuutwaa katika michuano kama hiyo iliyofanyika Uganda mwaka jana.


Msabi alisema, mbali na wachezaji wa timu za taifa za nchi husika, pia watashiriki kwenye michuano hiyowachezaji binafsi na wa vilabu kutoka nchi hizo.


"Leo tunafanya kazi ya 'droo' yaani kupanga timu zitakazoshiriki kwenye michuano, ambayo itafanyika hapa katika hoteli ya Moshi, Manzese", alisema Msabi.


Alisema, safari hii michuano hiyo inatarajiwa kuwa moto moto zaidi kwa kuwa wamepatiwa udhamini wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Safari Lager.


Hata hivyo alisema, licha ya timu yake kuwa na matumaini na ya kuibuka na aushindi, lakini haikukaa kambini kwa ajili ya maadalizi

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ยช