Na Mwandishi Maalum, New York
Baraza kuu la Umoja wa Mataifa limepitisha kwa kauli moja azimio linalohimiza Kuimarisha faida na Kuongeza kasi katika jitihada za kuuthibiti na hatimaye kuutokomeza Ugonjwa wa Malaria ifikapo mwaka 2015.
Mchakato wa majadiliano ya Azimio hilo yalihusisha nchi za Afrika kwa upande mmoja na nchi zilizoendelea kwa upande mwingine. Tanzania kupitia Ubalozi wake katika Umoja wa Mataifa, ndiyo iliyosimamia na kuendesha majadiliano hayo hadi kupatikana kwa Azimio hilo.
Akiwasilisha Azimio hilo mbele ya Baraza Kuu la 65 la Umoja wa Mataifa, Mwakilishi wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Ombeni Sefue amesema kwamba nchini nyingi zinazoendelea zikiwamo za Afrika zimeonyesha kufanikiwa katika kuudhibiti ugonjwa wa malaria.
Anasema mafanikio hayo ambayo kwa kiasi kikubwa yametokana dhamira ya kisiasa iliyoonyeshwa na viongozi wa nchi hizo, upatikanaji wa misaada kama vile fedha na madawa, pamoja na utambuzi wa haraka wa homa zitokanazo na malaria ukiwa umechangia sana.
Anasisitiza kuwa Suala la utambuzi wa haraka wa kutofautisha baina ya homa zitokanazo na vimelea vya malaria na homa ambazo hazisababishwi na vimelea vya malaria ni jambo la muhimu sana katika kuutibu na kuudhibiti ugonjwa huo.
Mwakilishi huyo wa Tanzania katika UM, amebainisha kuwa nchi nyingi zimefanikiwa katika upimaji na utambuzi wa homa zitokanazo na malaria,kutokana na ufadhili mkubwa katika eno hilo. Takwimu zinaonyesha kuwa kupitia ufadhili huo, utambuzi wa homa za malaria umeongezeka kutoka asilimia tano mwanzoni mwa mwongo huu hadi kufikia asilima 35 mwak 2009.
kwa namna yoyote ile anasema Balozi Sefue haya ni mafanikio tosha, ingawa bado kunahitajika uimarishaji na upanuzi wa uwezo huo wa kutambua ugonjwa wa malaria kutokana na ukweli kwamba matukio mengi ya malaria hayachunguzwi ipasavyo
Akielezea zaidi mafaniko katika kuudhibiti ugonjwa huo katika Afrika na nchi nyingine, Balozi Sefue anasema matumizi ya vyandarua vilivyotiwa viatilifu yameongezeka sana.
Kwa mfano anasema kati ya mwaka 2008 na 2010 zaidi ya vyandarua 289 milioni vyenyeviatilifu, vilikuwa zimesambazwa Kusini mwa Jangwa la Sahara.
Aidha inakadiriwa kuwa asilima 45 ya kaya katika Afrika zilikuwa zinamiliki angalau chandarua kimoja chenye viatilifu.
Kama hiyo haitoshi, asilimia 35 ya watoto chini ya miaka mitano wanalala kwenye vyandarua hivyo. “ haya ni mafanikio,lakini lengo letu la pamoja ni kuhakikisha kila mtu anapata chandarua kwa maana hiyo bado tunasafari ndefu”.
Aidha Tanzania kupitia Balozi Sefue imetaka kuwapo kwa uratatibu maalum utakaohakikisha kwamba ubadilishaji wa vyandarua ambavyo vimekwisha muda wake unafanyika kwa umakini bila ya kuathiri zoezi hilo.
Amesema uhai wa vyandarua vyenye viatilifu ni miaka mitatu na baada ya hapo nguvu ya dawa hiyo inakuwa imekwisha, sasa kama hapakuwapo na utaratibu mzuri wa kuvibadili kwa wakati kunahatari ya kurudhisha nyuma kazi nzuri ambayo imekwisha kufanyika hadi sasa.
Kuhusu matumizi ya dawa za mseto za malaria ( ACTs), Balozi Sefue anasema kutokana na nchi nyingi kubadilisha sera zake pamoja na kuongeza bajeti, nchi 11 za Afrika zimeweza kutoa dawa mseto kwa asilima 100 kwa wagonjwa waliokwenda kupata huduma katika sekta za umma hadi mwishoni mwa 2009.
Pamoja na mambo mengine Azimio hilo linasisitiza umuhimu wa kuimarisha miundombinu ya udhibiti na utokomezaji wa malaria ili kufikia malengo yakimataifa yaliyokubaliwa.
Aidha Azimio hilo inahimiza Jumuia ya Kimataifa, Umoja wa Mataifa na wadau wengine wote kushiriki kikamilifu katika ufadhili na utekelezaji wa mapango wa malaria duniani.
Wakati huo huo Msemaji wa Mpango wa Ushirikiano kuhusu Malaria ( Roll Back Malaria Partineship). Amesema Baraza Kuu kupitisha Azimio hilo, ni kielelezo kipya cha juhudi za nchi wanachama za kutekeleza malengo ya ushirikiano kuhusu udhibiti wa ugonjwa wa malaria na utekelezaji wa malengo ya maendeleo ya millennia.
Msemaji wa Ushirikiano huo, Bw Herve Verthoosel ameyasema hayo mara baada ya Baraza kupitisha Azimio hilo, huku akimpongeza Rais Jakaya Kikwete kwa kuonyesha dhamira ya kisiasa katika kukabiliana na Malaria na Ubalozi wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, kwa kusimamia azimio hilo na kuhakikisha kwamba linapita kwa kauli moja.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269