.

NMB YAZINDUA HUDUMA YA 'NMB PESAFASTA'

Apr 19, 2011

OFISA Mtendaji Mkuu wa  Benki ya NMB, Mark Wiessing (kulia) akizindua huduma mpya ya PesaFasta ya benki hiyo, jana kwenye hoteli ya Movenpick mjini Dar es Salaam. Huduma hiyo inawezesha mtu kutuma fedha kwa simu ya mkononi na mpokeaji akachukua fedha hizo kwenye tawi au mashine za ATM za benki hiyo hata kama hana akaunti au kadi ya ATM. Kushoto ni Mkuu wa Huduma binafsi za kibenki, abdulmajid Nsekela na wa pili ni Mkurugenzi wa ufundi wa kampuni ya FSDT , Sosthenes Kewe.
Mkurugenzi wa Ufundi wa kampuni ya Financial Sector Deepening Trust (FSDT), Sosthenes Kewe, akionyesha huduma ya NMB PesaFasta inavyotumiwa kwenye mashine ya kuchua fedha (ATM) wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo, leo. Kulia ni viongozi wa Benki ya NMB
Ofisa Mtendaji Mkuu wa benki ya NMB, Mark Wiessing akizungumza wakati wa uzinduzi huo
Meneja wa Masoko na Mawasiliano wa benki hiyo, Imani Kajula akizungumza wakati wa uzinduzi huo
Baadhi ya walioalikuwa kushuhudia tukio hilo la kihistoria.
Kundi la Tanzania House Of Talent (THT) likimbuiza katika hafla hiyo.
Hivi ndivyo unavyoweza kupata huduma hii.(Picha zote na http://www.chachandudaily.bogspot.com/)

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ª