.

USTAARABU WA BAADHI YA WAKAZI WA MAGHOROFA YA NHC DAR

Apr 19, 2011

Ukipitapita katikati ya jiji la Dar es Salaam, utashuhudia wakazi wa kwenye maghorofa kadhaa ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) wamening'iniza nguo ili zikauke baada ya kuzifua, kama hali hii iliyoshuhudiwa na Blogu hii katika Mtaa wa Mtendeni leo. Cha kushangaza ni kwamba licha ya kuwepo maghorofa mengi jijini, ni nyumba hizo tu za NHC zenye wakazi wenye tabia hiyo.

1 Comments:

William said...

Nakubaliana nawe kuwa tabia hii inaonekana sana katika hizi nyumba. Hata hivyo, unataka wakazianike nguo zao wapi? Majumba yenyewe haya yalijengwa karne iliyopita na wakaaji hawakuwekewa nafasi au mahali pa kuanikia nguo na hata kama una uwezo wa kuweka mashine ya kukaushia nguo, umeme je, na utaiweza hiyo gharama?

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ยช