Dk. Didas Masaburi zkizungumza na waandishi wa habari |
Tanzania (ALAT) utakaofanyika mei mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini Dar es Salaam,leo, Meye wa jiji hilo, Dk. Didas Masaburi alisema, mkutano huo wa siku tatu utafanyika katika hoteli ya Kunduchi Beach nje ya jiji.
Dk. Masaburi alisema mkutano huo ambao hufanyika kila mwaka, unatarajiwa kuhudhuriwa na Mameya 133
wa Halmashauri za Majiji,Manispaa, Miji na Wilaya, Wakurugenzu 133 wa Halmashauri na Wabunge 21 ambao ni mmoja kutoka kila mkoa.
Alisema, mkutano huo utahudhuriwa pia wajumbe kutoka wizara, Idara za Serikali Kuu, Wakala za serikali, Taasisi shiriki katika Serikali za Mitaa, wawakilishi wa mabalozi, wabia katika maendeleo, Mashirika ya Kimataifa na Jumuia za seriaki za Mitaa za Afrika Mashariki.
Dk. Masaburi alisema, kutokana na umuhimu wa mkutano huo, watahudhuria pia na asasi za kiraia, mashirika na kampuni na wawakilishi wa sekta binafsi na kwamba inakisiwa kuwa mkutano huo unahudhuriwa na washiriki 500.
Jumuia ya Tawala za Mitaa Tanzania ni chomvo kinachoziunganisha Halmashauri zote za wilaya, Miji,Manispaa na Majiji Tanzania bara ambapo kwa sasa zipo Halmashauri 133 ziinazounganishwa na chombo hicho.
Alisema kaulimbiu ya mkutano huo mwaka huu ni "Ubia baina ya sekta ya umma na jamii (PCP) ni nguzo muhimu ya kuleta maendeleo ya kijamii katika serikali za mitaa".
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269