.

MUKAMA AZUNGUMZIA UTEUZI WAKE: AAHIDI KUNG'OA MAKUNDI NDANI YA CHAMA

Apr 13, 2011

Katibu Mkuu wa CCM Wilson Mukama
KATIBU Mkuu mpya wa CCM, Wilson Mukama ameahidi kuvunja makundi ndani ya Chama na kwamba amepokea wadhifa huo kwa unyenyekevu mkubwa.


Akizungumza kwa mara ya kwanza na wafanyakazi wa makao makuu ya  CCM mjini Dodoma, Mukama aliahidi kufanyakazi kwa bidii na maarifa ili kurudisha imani ya wanachama na wananchi kwa CCM.


"Chama hiki ni kikubwa, chenye wanachama zaidi ya milioni tano...kuwepo migogoro ni afya, sehemu kubwa ya migogoro hii inachangia zaidi kujenga uhai wa chama na si kubomoa", alisema.


Aliahidi kuvunja makundi ndani ya chama akisema hayana nafasi na kwamba atatumia taratibu na kanuni za Chama kuhakikisha yanaondoka kabisa.


Mukama aliteuliwa katika Kikao cha Halmashasuri Kuu ya CCM, kilichofanyika mjini Dodoma, uteuzi uliofuatia kujiuzulu kwa Yussuf Makamba.


Pamoja na Makamba, sekretarieti yote na Kamati Kuu ya CCM nao walijiuzulu na nafasi zao zimeshajazwa.

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ยช