.

WATEJA WA STAR TIMES KULIPIA HUDUMA KUPITIA MASHINE ZA MAX-MALIPO AMBAZO HUTUMIKA KUUZA UMEME WA TANESCO

Apr 13, 2011


 Kaimu Mtendaji Mkuu wa  Star Media (Tanzania) Ltd,  William Lan  na
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Maxicom Africa, Juma Furaji,
wakitia saini mkataba huo,leo, kwenye Ofisi za Star Times, jijini.
KAMPUNI ya Maxcom Africa  imeingia mkataba wa kiabiashara na Star Media (T) Limited kwa wateja wa ving’aumuzi vya  Star Tmes kupata fursa ya  kulipia huduma hiyo kupitia mashine za MaxMalipo.

Mkataba huo ulitiwa saini jana mjini  Dar es Salaam kati ya Kaimu Mtendaji Mkuu wa  Star Media (Tanzania) Ltd,  William Lan (kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Maxicom Africa, Juma Furaji, kwenye Ofisi za Star Times ambapo walisema kuwa lengo ni  kufikisha huduma bora kwa kila mwananchi popote walipo.

Mkurugenzi wa Maxcom Africa, Furaji alisema  wateja wa Star Times kwa sasa wamepata mkombozi kwa kusogezewa huduma hiyo karibu ambapo inapatikana karibu kila kona ya Tanzania na kupata fursa ya kufurahia kuona chaneli za Star Times ambazo kwa sasa zinapatikana karibu sehemu kubwa ya nchi hii huku wakilipia kwa urahisi.

“Wateja watapata kulipia malipo ya Star Times popote pale walipo zilipo mashine za Maxcom Africa inayotoa huduma za MaxMalipo, kwa bei hilehile halisi na hakuna gharama za ziada hivyo wataendelea kufurahia maisha” alisema Furaji.

Furaji pia alisema, MaxMalipo imejizatiti kuendelea kutoa huduma bora na kuwafikia Watanzania ambapo watafurahia huduma hiyo kupitia mawakala 5000 ifikapo mwisho mwa mwaka huu kutoka mawakala 1200 waliopo sasa.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Star times  Lan alishukuru hatua hiyo ya makubaliano na kuwataka Watanzania kuendelea kuwaunga mkono katika huduma yao hiyo ambayo ni ya mfumo wa ‘Digital’ ambayo inasambazwa nchi nzima na wateja kufuraahia siku zote.

Maxcom Africa ni mawakala wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na inatoa huduma mbalimbali za malipo kupitia MaxMalipo ikiwemo huduma za Luku,VodaFone M-Pesa,Pay Tv Station DST na kwa sasa huduma hiyo ya Star Times.
Mwisho.
 

1 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ª