Breaking News

Your Ad Spot

Apr 13, 2011

NAPE AUNGURUMA DODOMA KUHUSU UFISADI, SEKRETARIETI YAO KUANZA ZIARA NCHINI

Na Mwandishi wa Chachandu Daily,  Dodoma .
Nape Mnauye


Katibu wa Itikadi na Uenezi (CCM) Nape Mnauye amesema yeyote atakayejaribu kupinga vita dhidi ya ufisadi inayofanywa na CCM atapambana na kuadabishwa vilivyo na nguvu mpya ya sasa ya chama hicho.

Nape amesema kama kuna kundi la watu au mtu mmoja mmoja ambaye anafikiri kuwa ataweza kujaribu
kuzuia vita hiyo anajidanganya kwa kuwa sasa CCM sasa imeamua na kamwe hakuna kundi nyuma au mtu
ambaye atazima vita hiyo.

“Ninachosaema ni kuwa kama kuna watu wanaofikiri wataweza kukishinda Chama safari hii wajaribu, sisi
tumeanza kazi na tunaendelea na tutamaliza na hakuna atakayekishinda chama kwani nguvu yake sa sasa ni
kubwa” alisistiza.

Katibu huyo aliwataka wanachama wa CCM ambao walihama chama hicho kwa hasira  au kutokana na
ufisadi uliopo warudi kwani sasa Chama ni kipya.

“Sasa tunajenga CCM mpya kwa mazingira na mahitaji ya wanachama hakuna sababu ya kununa tena.
Nimepata salaamu nyingi ya watu hasa vijana kutaka kurudi baada ya CCM kujivua gamba na sema
rudini”alisema na kuongeza kuwa kazi ya kijivua gamba kwa chama hicho itaendelea kwa awamu hadi kufikia ngazi zote kwa kuwa kama mtu anaamua kuoga ni vyema akaoga mwili mzima na si kuoga “Passport size”.

Alisema Sekretarieti Mpya ya Chama hicho itaanza kuwatembelea wanachama wao ikiongozwa na Makamu
Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Mzee Msekwa kwa kufanya  mkutano wake wa kwanza na wanachama mjini Dodoma kesho, katika viwanja vya Nyerere Square.

Nape alisema kushokutwa  Sekretarieti  hiyo itafika mjini Morogoro ambako itafanya mkutano wa hadhara na baadaye kwenda Chalinze  ambako Mwenyekiti wa CCM Taifa Rais Jakaya Kikwete aatakuwa miongoni mwa wananchi na wanachama wa CCM watakaoipokea sekretarieti hiyo.

Baada ya kumaliza hapo Chalinze Sekretarieti hiyo itaondoka siku hiyo hiyo kuelekea  Kibaha  na saa nane
mchana itakuwa Daressalaam na tarehe 17 Sekretarieti hiyo itaenda Zanzibar .

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages